Habari Mpya

Saturday, August 03, 2013

KAMA UNAO UWEZO, FANYA KITU KWA HUYU NDUGU, KABLA NAWE HAYAJA KUKUTA

MTOTO Ashura Mustapha (7) mkazi wa Mwandege, wilayani  Mkuranga, Pwani anasumbuliwa na ugonjwa wa kansa ya ngozi tangu akiwa na mwaka mmoja.  

 
Akizungumza na mwandishi wetu, baba mzazi wa mtoto huyo, Mustapha Makombe alisema kuwa mtoto wake anateseka na ugonjwa wa kansa ya ngozi tangu akiwa na umri wa mwaka mmoja.
 
Makombe alisema kuwa ugonjwa huo ulianza kama malengelenge akiwa na umri huo na wakawa wanaenda hospitali ndogo ndogo lakini baadaye wakaamua kumpeleka hospitali ya furaa ya Muhimbili ambapo walipewa barua yenye maelekezo kwenda hospitali ya CCBRT ambako ndiko walikogundua kuwa mtoto wake ana kansa ya ngozi hatua ya nne.

“Baada ya kuhangaika katika hospitali nyingi bila mafanikio, nikaamua kwenda Hospitali ya Regency (Dar) kuomba msaada wa kwenda kutibiwa India.
 
“Pale waliniambia nichangie shilingi milioni moja na laki tano kwa ajili ya tiketi na viza ili mwanangu akatibiwe India, hizo hela mimi sina. 
 
Naomba Watanzania mnisaidie hata kwa fedha za mitandao kwa namba 0769 517765 na 0715 424697 ili niweze kumpeleka mwanangu India akatibiwe,” alisema Makombe.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

0 comments:

Item Reviewed: KAMA UNAO UWEZO, FANYA KITU KWA HUYU NDUGU, KABLA NAWE HAYAJA KUKUTA Description: Rating: 5 Reviewed By: mcjohnminja.blogspot.com
Scroll to Top