Habari Mpya

Monday, October 21, 2013

WATU BILIONI MOJA WANAISHI CHINI YA MSTARI WA UMASKINI.


Watu bilioni 1 wanaishi chini ya mstari wa umaskini BENKI ya Dunia imetangaza kuwa watu bilioni moja duniani wanaishi chini ya mstari wa umaskini. 

Benki ya dunia hivi karibuni imetoa ripoti mpya kuhusu hali ya nchi maskini duniani ambapo masuala kama vile majanga ya kimaumbile na migogoro ya kiuchumi yamesab
isha kupungua kiwango cha misaada kwa nchi maskini duniani. 

Takwimu za Benki ya Dunia zinaonyesha kuwa katika idadi hiyo ya watu bilioni moja, kila mmoja ana pato la chini ya dola moja kwa siku na huishi kwa kutegemea senti 25 kwa siku. 

Benki ya Dunia imetahadharisha juu ya kuongezeka idadi ya watu maskini duniani na kuwasilisha stratejia mpya ya kupunguza kiwango cha watu maskini ulimwenguni. 

Kwa mujibu wa stratejia hiyo mpya, Benki ya Dunia inataraji kuwa umaskini utatokomezwa  ifikapo mwaka 2030 duniani.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

0 comments:

Item Reviewed: WATU BILIONI MOJA WANAISHI CHINI YA MSTARI WA UMASKINI. Description: Rating: 5 Reviewed By: mcjohnminja.blogspot.com
Scroll to Top