MUME ANAWEZA KUMFANYA MKEWE KUWA ZUZU!!!....SOMA HAPA!!!
Ni
wazi unawajua wanawake ambao wanaishi katika ndoa ngumu za manyanyaso
hadi unafikia kuuliza, ‘hivi huyo mwanaume amempa kitu gani kikubwa
hivyo?’ Wanawake hawa nao wanakuwa wamefikia mahali ambapo wanaamini
kuwa wanatakiwa kuishi hivyo, kwenye uhusiano wa ain hiyo.
Ni kitu gani kinatokea hadi mwanamke
kuamini kwamba yeye ameandikiwa kuishi kwenye ndoa ya shida na karaha
na mwingine kuamini kwamba hivyo ndivyo ndoa zinavyotakiwa kuwa? Malezi
na mazingira ni moja ya sababu kuu, lakini usugu ni sababu nyingine.
Ninaposema
usugu nina maana kwamba mwanaume anatokea kumdhalilisha mwanamke na
mwanamke huyo kuvumilia hadi anajikuta amefikia kuamini kwamba hiyo ndio
ndoa, hivyo ndivyo anavyostahili kuishi.
Mwanmke anapovumilia
mateso ya ndoa kwa muda mrefu sana bila kujua ni kwa nini au kwa
matarajio kwamba mmewe atabadilika, hufikia mahali ambapo kujiamini kwa
mwanamke huyo huisha na hujishusha kithamani na kuwa chini kabisa.
Hebu
jaribu kuwachunguza wanawake wote ambao wameteswa na kudhalilishwa kwa
muda mrefu na waume zao, unaweza kuona dalili fulani za uzuzu. Uzuzu huu
unatokana na mwanamke huyo kujishusha thamani kwa kuamini kwamba yeye
ni dhalili na si lolote.
Kumbuka kuwa hapa sizungmzii hali ambayo
tunaiita utegemezi, hali ambayo humfanya mwanaume au mwanamke kuona
kwamba hawezi kuishi bila kuwa na mwanamke au mwanaume aliye naye.
Hapa
nazungumzia ile hali ambapo hakuna utegemezi, bali mwanamke amekuwa
akijiambia kwamba mumewe atabadilika tu, bila jambo hilo kutokea.
Kwa
kuwa amevumilia kwa miaka kadhaa, hufikia mahali udhalilishaji huo wa
mwanaume ukamfanya mwanamke huyo kujishusha mwenyewe kithamani kwa
kutojiamini na kudhani kwa yeye ni mtu duni.
Hutokea vipi
mwanamke akawa zuzukufuatia kunyanyaswa au kudhalilishwa sana na mumewe?
Kinachotokea ni kwamba zile kauli na vitendo ambavyo anafanyiwa na
mumewe mara kwa mara kama sio kila siku, hatimaye hujijenga ndani mwake
na kumpa haiba mpya.
Haiba hii inakuwa ni ile ya kutojiamini,
kuogopa na kudhani yeye ni mtu duni, kwa sababu kauli na vitendo vya
mumewe dhidi yake vimejikita sana akilini mwake kiasi kwamba ameviamini.
Ni
vizuri kwa wanawake kuangalia tabia za wanaume ambazo kama wataamua
kuzivumilia kwa muda mrefu sana watajikuta wamekuwa mazuzu,wamekuwa ni
watu wasiojiamini, woga na wanaodhani wao ni duni.
Tabia hizi
zina athari kubwa za kisaikolojia kwa wanawake kutokana na ukweli kwamba
ni zenye uwezo mkubwa wa kutweza na kushusha hadhi ya anayeambaiwa au
anayetendewa.
Kuna wanaume ambao wana tabia ya wivu kupita kiasi,
wivu ambao hauna sababu za msingi. Kutokana na wivu huo wanakuwa ni
watu ambao wanajaribu sana kuwadhibiti wake zao kiasi kwamba wake hao
wanakuwa kama watoto wadogo kwao, wanakuwa kama mali ambayo inahitaji
kulindwa ili isiibwe au kupotea.
Hapa unaweza kukuta hata
mwanaume hufikia hatua ya kumkagua mkewe (watu wazima wanaelewa
nazungumzia ukaguzi upi) kila anaporudi nyumbani baada ya kutoka nje
kidogo hata kwa dakika kumi tu.
Kama unajikuta unaishi na
mwanaume mwenye tabia za unyanyasaji kama huo nilioutaja hapo juu,
inabidi uanze kukagua upya uhusiano wenu. Ni muhimu kuukagua upya kwa
sababu kama hilo litashindikana kuna uwezekano wa kuja kujikuta umezoea
maisha ya namna hiyo ambapo matokeo yake ni wewe kuwa zuzu.
0 comments:
Post a Comment