Habari Mpya

Thursday, February 20, 2014

Muswada wa Kupinga Ushoga Nchini Uganda ni Vita Ya Wahisani na Kanisa

Rais Yoel Museven ambaye ni Muumini wa Kanisa la "Evangelical Christian" ametangaza kuwa ataweka sahihi muswada wa kupinga Suala la Mapenzi ya Jinsia moja a.k.a Homosexual. Muswada huo ambao kwa mara ya kwanza ulianza kupata nguvu mwaka 2009 na watu mbalimbali nchi Uganda kuanza kujitokeza hadharani kwa ajili ya Kujitangaza kuwa wao ni waumini wa mapenzi ya Jinsia moja ulipelekea Rais Museven kuwapa Wataalam kazi ya Kuchunguza kama mapenzi ya Jinsia moja yana athari kwa Mwanadamu.
Wakati Wanasayansi hao wakiendelea na uchunguzi wao Kanisa la Nchini Uganda lilikuwa kwenye maombi kuhakikisha jambo hilo halipati kibari ndani ya nchi yao. Baada ya Wachunguzi kuwasilisha maoni yao kwa Rais, Ulimwengu Mzima ulikuwa ukisubiria kauli ya Rais huyo angesema nini, pasipo kumung'unya maneno akautangazia ulimwengu kama misaada basi bora akose ila atakayepatikana anafanya mapenzi ya Jinsia moja basi gereza la maisha litakuwa likimsubiria. Rais Obama pamoja na Waziri Mkuu wa Uingereza wameachwa na butwaa kwa kuwa wao ni kati ya Watu wanao support mapenzi ya Jinsia moja.
Kitendo hiki ambacho kinaonekana ni Ushindi kwa Kanisa la Uganda limechora rasmi mstari wa uhasama kati ya Kanisa hilo na Wahisani wa nchi za Magharibi ambao wao suala la ndoa za jinsia moja na mapenzi ya jinsia moja ni haki ya binadamu inayotambulika.
Ikumbukwe Juzi kati Rais Wa Jamuhuri ya Muungano Wa Tanzania alipokuwa nchini Uingereza aliulizwa swali kama anadhani Watanzania Wako tayari kuruhusu Ushoga na Usagaji, Rais wetu akasema "hadhani kama tuko tayari kwa hilo kwa sasa.
Sources: http://en.wikipedia.org/wiki/Uganda_Anti-Homosexuality_Bill

              http://www.sbs.com.au/news/article/2014/02/17/uganda-president-sign-anti-gay-bill

             http://www.bbc.co.uk/news/world-africa-20754891

               http://www.bbc.co.uk/news/world-africa-20754891
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

0 comments:

Item Reviewed: Muswada wa Kupinga Ushoga Nchini Uganda ni Vita Ya Wahisani na Kanisa Description: Rating: 5 Reviewed By: mcjohnminja.blogspot.com
Scroll to Top