Wandugu leo hii naomba
tuzungumzie jambo moja la kuweza kumtambua mtu aliyegombana na mwenzake kwa
kupitia mawasiliano yao….
Siku zote palipo na
upendo utajua tu kwa kuangalia au kusikia namna ya maongezi yao
wanavyowasiliana, huwa ni kwa upole na tabasamu lenye kudhihirika waziwazi,
tena usipokuwa makini hauwezi kusikia wameongea nini….. ukiona hivyo ujue
upendo umetawala kwa kila mmoja au kwa mmoja wao kati ya hao waongeao.
Lakini sasa, Siku zote
huwezikuta waliogombana wakiongea kwa upole, na kwa sauti ya chini… mara nyingi
wengi wao hujikuta wanaongea kwa kupayuka tena kwa sauti kubwa, na haijalishi wapo umbali kihasi gani au karibu
kihasi cha kugusana.
Kwa udhirisho huo ndiyomaana
nawezakusema unaporuhusu ugomvi kuzidi
kuwa mkubwa kwako, ni dhahiri kabisa
ndivyo umbali wa kisaikolojia unavyozidi kuongezeka kati yako na uliyegombana
naye, pasipo wewe mwenyewe kuuona huo
umbali, na hautokuja kuuona huo umbali mpaka utakaporuhusu element za upendo
ndani yako… nipo taratiiiibu utajikuta unaanza kupunguza umbali uliopo kati
yake na Yule au wake aliyogombana nao.
Embu kuanzia sasahivi
jiangalie katika maongezi unavyowasiliana na watu wengine, na utakapojikuta
unaongea na mtu kwa sauti kubwa na mtu huyo yupo karibu kiasi cha kuweza
kumuongelesha kwa sauti ya chini na mkaelewana, itadhihirisha wazi kuwa kuna
shida kati yako na Yule unayewasiana naye.
JITAHIDI KUEPUKA
UGOMVI…. IMARISHA UPENDO …… PENDANA NA WATU….KUDUMISHA AMANI
0 comments:
Post a Comment