Mpita njia akipita kwenye lundo la theluji iliyowekwa pembeni baada
ya magari ya plao kuisogeza kwa ajili ya kusafisha njia ya magari ili
yaweze kupita bila matatizo yeyote, theluji iliyoanguka DMV ni kuanzia
inchi 8, mpaka 18 na majimbo mengine yaliyoathirika na theluji hii ni
pamoja na North Carolina, Alabama, Georgia, kwa wanaosafiri leo
wanatakiwa wawe waangalifu na kama huna safari ya uzalima umeshauliwa
utulie nyumbani kama kama utalazimika kutoka hakikisha unamafuta ya
kutosha kwenye gari na wanaosafiri na anga unatakiwa upige simu kwanza
kwa sababu usafiri wa anga sehemu nyingi umesitishwa.
Maeneo ya Beltsville, Maryland katika picha.
Maeneo ya I 95 N yalivyokua yakionekana leo baada ya theluji kuanguka usiku wa kuamkia leo Alhamisi maeneo ya DMV
Pamoja na kwamba hakuna kazi sehemu nyingi zikiwemo ofisi za
serikali na shule magari ya kubebea wagonjwa yapo kazini kama kawaida
zikiwemo sehemu muhimu kama mahospitalini na kwengineko.
Maeneo Denton, Maryaland.
Barabara nyingi kubwa wamejitahidi sana kusafisha.
Juu na chini ni maeneo ya Denton wakaazi wakijaribu kuondoa theluji
iliyozuia magari yao yalio kwenye maegesho ya nyumba wanazoishi
credit : Vijamambo blog
0 comments:
Post a Comment