Habari Mpya

Friday, November 21, 2014

Kiburi ni sifa ya Shetani

Dada alikuwa airport akisubiri connetion ya ndege yake, wakatangaziwa ni 2 hr swaiting time.

Akaamua kununua gazeti na box Dogo la biscuits, akatafuta sehemu akakaa kusoma gazeti kusubiri muda ufike wa kuingia kwenye ndege, alipokaa pembeni yake kulikuwa na kaka nae anasoma gazeti akisubiri ndege.

Dada alishangaa alipokuwa akitoa biscuit kwenye box aliloliweka pembeni yule kaka nae anachukua moja anakula, akamwangalia kwa hasira, kaka akawa anatabasamu.
Dada akakasirika akataka kumtolea maneno machafu akajizuia. Ukawa
mchezo kila dada akichomoa biscuit moja yule kaka nae anachukua moja.


Ikaendelea hadi ikabakia biscuit moja. Yule kaka akawahi kuichukua akaimega nusu akampa yule dada, ...dada kwa ghadhabu akanyanyuka akamtukana sana yule kaka na maneno ya kumdhalilisha kwanini anavamia vitu vya watu asinunue vyake!! Kaka alikaa kimya bila kumjibu yule dada.

Mara wakatangaziwa muda wa kuingia kwenye ndege, yule dada akaingia
akimuacha kaka nae akisubiri ndege yake. Alipokaa kwenye siti yake
akafungua mkoba aweke simu yake, mara alishtuka kuona box lake la
biscuits zima wala halijafunguliwa, kumbe alikuwa anakula biscuits za yule
kaka. Akajutia sana akatokwa na machoz jinsi alivyomdhalilisha yule
kaka, na muda wa kurudi kuomba msamaha haupo tena kwani milango ya
ndege ilishafungwa na kuanza kuondoka.

"Muda wa kuomba msamaha kwa uliyemkosea upo usisubiri milango
ifungwe"...



Kiburi ni sifa ya Shetani

Kwa Hisani ya. Ney Msuya Wa Francis
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

0 comments:

Item Reviewed: Kiburi ni sifa ya Shetani Description: Rating: 5 Reviewed By: mcjohnminja.blogspot.com
Scroll to Top