siku zooote dawa chungu ndiyo inayoponya magonjwa, mfano maleria dawa zake lazima ujipange kutafuta juice.
Wewe mdada kama Ukijaliwa
kuwa Msichana mzuri na mrembo,usidhani utatetemesha kila Mwanaume, kuna
wanaume na akili zao kichwani,
urembo wako hauwasumbui,kama bichwa lako
ni kanyaboya,uzuri wako hausaidii kitu,na utashangaa no one is
paying attention,
watu utakaowapata ni walewale kanyaboya wenzako, na hawana future utabaki unaliwa bure kila siku unatolea macho mimi ndiyo nakwambia ukweli sasa.
Ukipata mwanaume anakupenda unaanza drama zako na kupiga watu danadana,madai yako hujali na unadhani hata akiondoka utapata mwingine kisa wewe ni mzuri,la hasha!
Mwanaume akijitoa mhanga kukupenda kwa uzuri wako mheshimu,maana viumbe wa kike
wakiwa wazuri ni shida na matatizo na sasa ujue kabisaaa hakuna mtu anataka kumuowa mke mreeembo, kwani tunatambua nyie ni pasua kichwa sana!!!!
ukimwongezea na drama pamoja na yeye kujigeuza mpalestina kwako utajikuta umeolewa na kioo cha chumbani kwako, maana hicho ndo kinakudanganya sana kwamba we eti ni mrembo,
Watch out, drama zina mwisho, leo unacheza na mioyo ya watu unajiona we kifaa,usidhani wanaume hawaumii, tunaumia sema hatusemi tu,machozi yetu kama ya
samaki, tunalia ndani kwa ndani.
0 comments:
Post a Comment