Imeripotiwa
kuwa asilimia 80 wanatoka Barani Afrika, ambako Nigeria ni ya kwanza,
ikifuatiwa na Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo na ya tatu ni Angola
ikifuatiwa na Tanzania inashika nafasi ya nne kwa kuwa na idadi kubwa ya
wagonjwa ambapo kila mwaka watoto 10,000 uzaliwa na siko seli.
Akielezea
kuhusiana na ugonjwa huu Mtaalam wa magonjwa ya watoto nchini Nairobi
Aghakan Hospitali, Dr Wafulla Kennedy Charles alisema ugonjwa unahusu
damu hasa kwa chembechembe hai kuganda na kuzuia damu kupita hivyo
kusababisha mishipa kuziba na sehemu ambazo zinapokea damu kushindwa
kupata hewa na chakula hali inayopelekea mgonjwa kuhisi maumivu
Aidha
Dr. Charles alisema Ugonjwa huu uanza kuonekana kutokana na
chembechembe ndogo za damu kushindwa kufanya kazi, chanzo chake ni
wazazi iwapo watakuwa na vinasaba vya siko seli na mtoto kuchukua
vinasaba hivyo ndipo ugonjwa huo hutokea na hiyo huitwa siko seli anemia kurithi kutoka kwa wazazi.
Ni zipi dalili za ugonjwa wa siko seli?
Mara
nyingi dalili za ugonjwa huu hutegemea na kiwango cha uathirikaji wa
chembe chembe nyekundu za damu, miongoni wa dalili hizo ni upungufu wa
chembechembe za damu mwilini, kizunguzungu pamoja na maumivu makali ya
kichwa
Naye
Bi. Faudhia Juma Mkazi wa Manispaa ya Morogoro ni mama wa watoto ambao
wana matatizo ya siko seli akitoa ushuhuda amesema ugonjwa huo umeanza
kuonekana kwa watoto wake walipofika umri wa miezi tisa.
“Mwanzo
ilikuwa ni ngumu kugundulika na kupatiwa tiba lakini baadaye
ikagundulika kuwa ni siko seli hivyo watoto wangu wote wawili wana
tatizo la siko seli tatizo ambalo walilipata kutokana na kurithi toka
kwetu” alisema Bi Faudhia
Je ni madhara gani ambayo anaweza kupata mgonjwa wa siko seli?
Madhara
ambayo mgonjwa anaweza kupata kutokana na ugonjwa wa siko seli ni
kukabiliwa na maambukizi ya bakteria mwilini na Kiarusi.
Kwa
upande wake Dr. Yusuph Almasi wa Idara ya Afya Mkoa wa Morogoro
alibainisha kuwa ugonjwa huo ni wa kudumu hauna matibabu ya kuponya
kabisa bali kinachofanyika wagonjwa wanapopata maumivu wanapewa dawa ya
kutuliza maumivu hayo (Antpain)
Aliongeza
kuwa wagonjwa hawa ni rahisi sana kupata magojwa tofauti kama Maralia,
Nimonia na ni vema endapo anapata ugonjwa huu apewe tiba haraka kwa kuwa
wagonjwa hawa hawana kinga yenye nguvu ya kupigana na magonjwa tofauti
kama watu wengine
“Ni
kawaida kwa mgonjwa wa Siko Seli Anemia kupata upungufu wa damu hivyo
wanalazimika kuongezewa damu ili kurudi katika hali ya kawaida na ikiwa
damu inapungua kwa wingi wanatakiwa wapewe chanjo, chanjo hiyo ni muhimu
sana kwa kila mtoto lakini kwa watu wa siko seli ni muhimu zaidi”
alisema Dr.Almas.
Aidha
Dr. Almas alisema imegundulika kuwa tatizo kubwa linalowakabili mara
kwa mara wagonjwa wa Siko Seli ni nimonia, hivyo wagonjwa hao wanatakiwa
kupata chanjo ya nimonia inayoitwa ‘nimokokobadseed’ kwa maana ya kuwapunguzia shambulio la ugonjwa huo
Unawezaje kupambana na ugonjwa wa siko seli?
Hata
hivyo mwenyekiti wa mfuko wa Seli nchini Tanzania Grace Rubambey
amesema hakuna tiba ya moja kwa moja mahsusi kwa ugonjwa wa siko seli
hivyo matibabu hutofautiana kulingana na jinsi ugonjwa huo
ulivyomuathiri mgonjwa, kuna wengine huongezewa damu, kuongezewa maji na
hata wengine kupewa dawa za kutuliza maumivu.
Pia
Rubambey amesema watoto wenye ugonjwa huu wanatakiwa wapewe chakula
kilicho bora kutokana na magonjwa haya yanayowanyemelea mara kwa mara
hiyo itasaidia kurudisha afya zao
Ameongeza
kuwa wakati mwingine wagonjwa hawa wanaweza kupata ugonjwa wa kupooza
(strock) ambapo itawalazimu madaktari kuwaongezea damu kila mwezi mara
moja ili kuzuia wasipate ugonjwa wa kukupooza (strock) kwa mara nyingine
kwani wakipata ugonjwa huo kwa mara ya pili au ya tatu ni rahisi
wakapoteza maisha yao.
Aidha
wanandoa watarajiwa wanatakiwa kupima ugonjwa huu kabla hawajaamua
kuzaa watoto ili kuepuka uwezekano wa kuzaa watoto wenye ugonjwa wa siko
seli na kuwapa tabu katika maisha yao hivyo ni vema kuchukua hatua
kwanza kwa kizazi kilicho salama.
Je nini sababu ya kukua kwa ugonjwa wa Siko Seli Tanzania?
Kwa
upande wake Mratibu wa Kitengo cha Seli Mundu kutoka Hospital ya Taifa
Muhimbili (MNH) Dr. Deogratius Soka amesema sababu kubwa inayofanya
ongezeko kubwa la idadi ya watoto wenye ugonjwa wa siko seli ni kutokana
na ufinyu wa uelewa kuhusiana na ugonjwa huo
Pia
amesema kuwa asilimia 15 ya watanzania wanavinasaba vya ugonjwa wa siko
seli hivyo juhudi za makusudi zinatakiwa zifanyike kwa jamii kupatiwa
elimu kuhusiana na ugonjwa huo.
Dr. Soka ameendelea kusema kuwa idadi kubwa ya wagonjwa wa Siko Seli nchini wanapatikana katika Mikoa ya Tanga , Dar es Salaam, Pwani, Mara Mwanza, Bukoba, Shinyanga Tabora na Dodoma.
Kufikia
hapa tumefikia tamati ya makala haya, hakika umeweza kuona ugonjwa wa
Siko Seli maana yake na umeona jinsi unavyoambukizwa, pia tumeona njia
ya kuweza kukabiliana nao japo kuwa hauponi, tukutane tena wiki ijayo
katika Makala nyingine ya Afya.
kwa hisani ya Taty (Sua Media)
0 comments:
Post a Comment