Habari Mpya

Thursday, February 18, 2016

Njia Ipo Ukiitafuta

Good Morning.
Kwenye maisha kuna wakati utajikuta unalazimika kuanza upya baada ya kile ulichokuwa nacho kupotea ama ulichotarajia haujakipata.

Nimesoma habari za wengi na nimekutana na watu wengi sana ambao walifanikiwa kuanza upya na kutimiza malengo yao baada ya kupitia hali ngumu maishani mwao.Kuna mtu alipoteza familia yake yote Kwenye ajali akabaki peke yake akaona kama vile maisha yamefika mwisho lakini baada ya kuwa tayari kuanza upya na kukubaliana na yaliyotokea leo ameweza kuyashinda maumivu yote na amefanikiwa kufikia ndoto yake.

Baada ya kushindwa kuendelea na shule na kujikuta akiishi maisha ya mtaani baada ya wazazi wake kuachana akiwa na umri wa miaka 7 alikubali kuanza upya na leo Anthony Robins ana utajiri takribani dola za kimarekani 400m,anamiliki ndege, majumba makubwa etc .

Baada ya kupitia mateso na uchungu wa kubakwa akiwa na miaka 14  na kukataliwa mara nyingi alipoenda kutafuta Kazi za utangazaji,Leo Oprah Winfrey sio tu anatangaza bali anamiliki vyombo vya habari,ALIAMUA KUANZA UPYA.

Baada ya Steve Jobs kufukuzwa Kwenye kampuni ambayo aliianzisha yeye mwenyewe,hakukata tamaa ya kutimiza ndoto yako.ALIAMUA KUANZA UPYA.

Umefeli mtihani,umeachwa na umpendaye,biashara yako imefilisika,umepoteza kila ulichonacho,umefukuzwa kazi...Usikubali kukaa chini na kuanza kulia.AMUA KUANZA UPYA LEO.

Naona ndoto yako ikitimia, naona ukiwasaidia wengi kufanikiwa kutokana na historia yako,naona ukiinuka na kuwainua wengi watakaopitia hali kama uliyopitia.

Naamini Katika ndoto yako,
Naamini Katika Uwezo Wako,
Naamini Katika Hatima Yako.

By Joel Nanauka
See You At the Top.
Tembelea (www.JoelNanauka.Com)  Ujifunze Zaidi
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

0 comments:

Item Reviewed: Njia Ipo Ukiitafuta Description: Rating: 5 Reviewed By: mcjohnminja.blogspot.com
Scroll to Top