Habari Mpya

Tuesday, March 01, 2016

DARASA LA ALHAMIS na DR. CHRIS MAUKI: TABIA ZA WATU WALIOFANIKIWA AU WENYE MAZINGIRA YA KUJA KUFANIKIWA

Kufanikiwa ni kiu ya kila mmoja ingawa ukweli ni kwamba wengi wetu tunabaki tunayatamani mafanikio wakati hatuna mazingira yeyote ya kuruhusu mafanikio hayo yawepo au yatujie. 

Mr. Chris Mauki

Hapa nakuletea tabia za watu wawili tofauti, mmoja akiwa ni mtu mwenye mafanikio au yule ambaye ana mazingira ya kuja kufanikiwa na mwingine ni mtu asiye na mafanikio na asiye na mazingira ya kufanikiwa maishani. Nitaanza na tabia za watu wenye mafanikio;

1. Ni watu wenye kushukuru kwa kila jambo, sio wenye kutoa lawama

2. Ni watu wenye tabia ya kupongeza pale wanapoona mwingine anastahili pongezi

3. Ni watu wenye tabia ya kusamehe, tena wanasamehe kwa urahisi wala sio kwa kuombwa na kulazimishwa

4. Ni watu wasioona uchungu kuwapongeza wengine au kukubali wengine wanapopata ushindi wa aina yeyote, na sio tu kuwapongeza bali pia hawaoni ugumu kuwasaidia au kuwashauri wengine ili wafanikiwe zaidi

5. Ni watu wanaokubali wakati wote kubeba majukumu au lawama pale wanaposhindwa kufanya inavyopaswa, sio wenye kujitetea au kujaribu kukwepa majukumu

6. Ni watu wenye tabia ya kupenda kusoma kitu kila siku, sio wavivu wa kusoma au kutafuta taarifa na ujuzi

7. Ni watu wenye tabia ya kuweka utaratibu wa nini kinafanyila leo na nini kitafanyika kesho na kwa nini kifanyike, sio watu wanaoburuzwa na mazingira yanaowazunguka au kuendeshwa na marafiki zao

8. Sio watu wenye kuzungumza sana kuhusu watu wengine na madhaifu yaw engine bali ni wenye kuzungumza zaidi kuhusu mawazo ya kujenga au mawazo ya kimaendeleo

9. Mara zote wana kiu ya kuona wengine wanafanikiwa, hata kama mafanikio hayo yatayazidi yale wao walionayo

10. Sio wachoyo katika kutoa taarifa au ujumbe wowote muhimu kwa mtu yeyote, maana wao hawana uchungu na mafanikio au ushindi wa mwingine

11. Ni watu wenye kuonyesha furaha wakati wote, sio wenye kununa, kuzira na kuwa na huzuni mara kwa mara

12. Ni watu wanaoweka malengo na kuongozwa na malengo katika maisha yao ya kila siku, sio wanaokurupuka kufanya mambo kwa hisia, misukumo au mashindano tu

13. Sio waoga wa mabadiliko, bali hutamani mabadiliko chanya na yenye kujenga na kuleta maendeleo, na kwahiyo mara zote kuyawezesha mabadiliko kutokea kwao na kwenye maisha ya wengine na sio kuyapinga

14. Kwao kujifunza ni tabia endelevu sio jambo linalotokea wakati wakiwa shuleni tu, wao huhesabu maisha ya kila siku ni kama shule

15. Kiu na msukumo wa maisha yao ya kila siku ni katika kusababisha mabadiliko, aidha mabadiliko kwao wao binafsi au kwa wale wanaowazunguka. KWA HISANI YA CHRIS MAUKI 





MUHIMU KWAKO....!!!
kama wewe ni mtafutaji wa kujitegemea au unatarajia kuja kuwa.... zingatia hii

JOINT SCOPE LTD imedhamiria kutoa msaada wa ushauri bure, kwa wanaotarajia au wanataka kusajili BUSINESS NAME au COMPANY LIMITED n.k.
 
hapa utaelezwa mchakato mzima na kila kinachohitajika wakati utakapotaka kufanya usajili wa kampuni au Jina la Biashara kupitia Brela, ambayo ndiyo mamlaka pekee Tanzania yenye mdhamana ya kusajili Kampuni (Company LTD) na Jina la Biashara (Business Name), Logo n.k.
 
Tumeamua kutoa huduma hii ya ushauri bure kutokana na kero za matapeli tulizokutana nazo na tulishindwa kuwatambua kutokana  na kutoweza watambua kwa kutojua ukweli halisi wa vinavyohitajika wakati wa usajili wa Kampuni ya JOINT SCOPE LTD.
 
"Ni vyema Kutafuta Elimu ya Jambo Unalotaka Kufanya Kwanza Kabla ya Kuanza Kufanya"

Kwa Mawasiliano
Simu: 0712 479 905

E-mail; jointscope@gmail.com

P.O. Box 2574 Morogoro - Tanzania

Huduma hii ni Bure kwa watanzania Tu!

ToGether We Can.....!!!!!
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

0 comments:

Item Reviewed: DARASA LA ALHAMIS na DR. CHRIS MAUKI: TABIA ZA WATU WALIOFANIKIWA AU WENYE MAZINGIRA YA KUJA KUFANIKIWA Description: Rating: 5 Reviewed By: mcjohnminja.blogspot.com
Scroll to Top