Balozi
wa kampuni ya StarTimes Tanzania kwa upande wa vipindi na chaneli za
michezo, Bw. Shaffih Dauda (katikati) akionyesha nambari ya smati kadi
ya mshindi wa tano na wa mwisho wa safari ya kwenda Ujerumani.
Wakishuhudia tukio hilo ni Meneja Mauzo wa kampuni hiyo, Bw. David
Kisaka (kushoto) na Mkaguzi kutoka Bodi ya Michezo ya kubahatisha
Tanzania, Bi. Chiku Salehe (kulia). Katika droo hiyo pia StarTimes
walitangaza ofa ya punguzo la bei kipindi hiki cha Pasaka kwa kushusha
bei ya visimbuzi pamoja kufurahia vifurushi vya kawaida na cha michezo
cha Sport Plus.

michezo, Bw. Shaffih Dauda (wa kwanza kulia) akimpigia simu mshindi wa
tano na wa mwisho wa safari ya kwenda Ujerumani. Wakifuatilia tukio hilo
kutoka kushoto ni Mkaguzi kutoka Bodi ya Michezo ya kubahatisha
Tanzania, Bi. Chiku Salehe, mfanyakazi wa StarTimes kutoka kitengo cha
maudhui, Bw. Daniel Msangi na Meneja Uhusiano, Bw. Muddy Kimwery. Katika
droo hiyo pia StarTimes walitangaza ofa ya punguzo la bei kipindi hiki
cha Pasaka kwa kushusha bei ya visimbuzi pamoja kufurahia vifurushi vya
kawaida na cha michezo cha Sport Plus.
Balozi
wa kampuni ya StarTimes Tanzania kwa upande wa vipindi na chaneli za
michezo, Bw. Shaffih Dauda (kushoto) akimpigia simu mshindi wa tano na
wa mwisho wa safari ya kwenda Ujerumani. Wakifuatilia tukio hilo kutoka
kulia ni Mkaguzi kutoka Bodi ya Michezo ya kubahatisha Tanzania, Bi.
Chiku Salehe, mfanyakazi wa StarTimes kutoka kitengo cha maudhui, Bw.
Daniel Msangi na Meneja Mauzo wa kampuni hiyo, Bw. David Kisaka. Katika
droo hiyo pia StarTimes walitangaza ofa ya punguzo la bei kipindi hiki
cha Pasaka kwa kushusha bei ya visimbuzi pamoja kufurahia vifurushi vya
kawaida na cha michezo cha Sport Plus.
Balozi
wa kampuni ya StarTimes Tanzania kwa upande wa vipindi na chaneli za
michezo, Bw. Shaffih Dauda (wa kwanza kulia) akiongea kwa njia ya simu
na mshindi wa tano na wa mwisho wa safari ya kwenda Ujerumani. Katika
droo hiyo pia StarTimes walitangaza ofa ya punguzo la bei kipindi hiki
cha Pasaka kwa kushusha bei ya visimbuzi pamoja kufurahia vifurushi vya
kawaida na cha michezo cha Sport Plus.
Meneja
Mauzo wa kampuni ya StarTimes Tanzania, Bw. David Kisaka (kushoto)
akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati wa droo ya
tano na ya mwisho ya safari ya kwenda Ujerumani. Katika droo hiyo pia
StarTimes walitangaza ofa ya punguzo la bei kipindi hiki cha Pasaka kwa
kushusha bei ya visimbuzi pamoja kufurahia vifurushi vya kawaida na cha
michezo cha Sport Plus. Akimsikiliza kwa makini kulia ni Meneja
Uhusiano, Bw. Muddy Kimwery.

………………………………………………………………
Na Dotto Mwaibale
Kampuni
ya StarTimes imezindua ofa bab-kubwa kwa wateja wake wote nchini kwa
kushusha bei ya visimbusi vyake vya antenna na dishi pamoja na kuwapatia
ofa ya kutazama kifurushi cha michezo cha Sport Plus mwezi mmoja bure
kabisa.
Akizungumza
na waandishi wa habari wakati wa uzinduzi huo ulioambatana na
uchezeshwaji wa droo ya mwisho ya kusijishindia safari ya Ujerumani
kutazama mechi ya Bundesliga Meneja Masoko wa kampuni hiyo, Bw. David
Kisaka ameeleza kuwa ofa hiyo ni maalum kusindikiza shamrashamra za
sikukuu za Pasaka.
“Leo
nina habari njema kwa wateja wetu kwamba kuisha kwa promosheni ya
kujishindia tiketi ya kusafiri Ujerumani kutazama mechi ya Bundesliga
‘live’ imefikia ukingoni siku ya leo. Ningependa kuchukua fursa hii
kumpongeza mshindi wetu wa mwisho Bw. Makame Kundi Makame kutoka
visiwani Zanzibar na kutufungia pazia ya promosheni hiyo. Lakini kama
tulivyokwisha waahidi wateja wetu kwamba mwisho wa promosheni hii ni
mwanzo wa promosheni nyingine ya Pasaka.” Alisema Bw. Kisaka
“Katika
kipindi hiki cha kuelekea kwenye shamrashamra za Pasaka tungependa
kuwataarifu wateja wetu na watanzania kwa ujumla kuwa tumeshusha bei ya
visimbuzi vyetu. Vya antenna vitapatikana kwa shilingi 22,000/- tu
pamoja na mwezi mmoja wa bure wa vifurushi vya Mambo na cha michezo cha
Sport Plus. Na wateja wa dishi watajipatia kwa shilingi 46,000/- pamoja
na mwezi mmoja wa kifurushi cha Smart na Sport Plus.” Aliongezea Bw.
Kisaka
Meneja
huyo wa Masoko amefafanua kuwa ofa hizo ni kutaka kuwaonyesha ni jinsi
StarTimes imejizatiti kwa chaneli na vipindi vya michezo hususani mchezo
wa soka unaopendwa na watanzania wengi. Kwa kupitia punguzo hilo la bei
anaamini kuwa sasa huduma zao zitapatikana kwa urahisi na kufurahiwa na
kila mtu.
“Kupitia
ofa ya mwezi mmoja ya kifurushi cha Sport Plus chenye chaneli za Sport
Life, Sport Premium na Worl Football zinazoonesha ligi za Bundesliga na
Serie A moja kwa moja ninaamini Pasaka hii itakuwa ni shangwe tupu. Kwa
wateja wetu ambao tayari wanavyo visimbuzi vya antenna na dishi pia
hatujawasahau kwani wao wakilipia vifurushi vya mwezi vya Mambo na Uhuru
pamoja na Smart watapata mwezi mmoja bure wa kifurushi cha Sport Plus
na vile vile watakaolipia vifurushi vikubwa va Kili na Super watapatiwa
wiki moja zaidi ya vifurushi hivyo.” Aliongezea Bw. Kisaka
“Ningependa
kuwapongeza washindi wetu wote waliojipatia fursa ya kushinda safari ya
Ujerumani, ninaamini watafurahia safari yao. Pia ningetoa wito kwa
wateja na watanzania kwa ujumla waichangamkie fursa hii ya punguzo la
bei na kufurahia mechi za Bundesliga na Serie A kupitia kifurushi cha
Sport Plus. Kwa bei ya sasa ninaamini hakuna atakeyekosa kisimbuzi chetu
wala kutofurahia mechi hizo za ligi za Ulaya.” Alihitimisha Meneja huyo
Mshindi
katika droo hiyo mwisho, Bw. Makame Kundi Makame mwenye umri wa miaka
43 ni mkazi wa Unguja visiwani Zanzibar na anajishughulisha na shughuli
za hotelini.
Akizungumza
kwa njia ya simu alisema kuwa amefurahishwa sana na promosheni hiyo
kwani mara nyingi kampuni zingine huwahusisha wateja wao waliopo Dar es
Salaam pekee. Lakini mpaka yeye kupigiwa simu alisema kweli kwa hakika
StarTimes iliposema promosheni hiyo ni kwa wateja wao wan chi nzima
ilikuwa ikimaanisha.
Bw.
Makame anaungana na washindi wengine wanne waliopita ambao ni Profesa
Bernadeta Killian wa Iringa, Bi. Kisa Uswege wa Mbeya, pamoja na Bw.
Yohanes Maluli na Bw. Joseph Mogela wote wa jijini Dar es Salaam. Hivyo
baada ya droo hiyo kukamilika washindi hao wanasubiri safari yao ya
kwenda Ujerumani ambayo inatazamiwa kuwa mwezi ujao wa Aprili.
(Imeandaliwa na mtandao wa www.habari za jamii.com-simu namba 0712-727062)
(Imeandaliwa na mtandao wa www.habari za jamii.com-simu namba 0712-727062)
0 comments:
Post a Comment