Siku ya Wanawake ilianza mwanzoni mwa miaka ya 1900 kwa kupitia wanawake wafanyakazi wa sekta ya viwanda nchini Marekani walioandamana kupinga mazingira duni ya kazi zao, walilalamikia ukosefu wa huduma za kijamii na kuwepo kwa vitendo vya unyanyasaji katika ajira. Kutokana na hali hiyo, nchi ya Marekani ilikubali kuwa na siku ya maadhimisho ya kitaifa ili kutafakari masuala mbalimbali yanayohusu haki na ustawi wa wanawake.
Baadaye Umoja wa Mataifa ulipaoanzishwa mwaka 1945,ilipofika
tarehe 8 Machi iliridhiwa iwe Siku ya Kimataifa ya Wanawake Duniani. Uamuzi huo
wa Umoja wa Mataifa ulitokana na kukubali kwake kwamba masuala ya haki,
maendeleo na usawa wa wanawake yalihitaji msukumo maalumu na wa pekee.
Madhumuni ya kuadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani ni
kuwezesha jamii kupima utekelezaji wa maazimio, matamko, mikataba na itifaki
mbalimbali za Kimataifa/ kikanda na kitaifa zinazohusu masuala ya
maendeleo ya jinsia na wanawake katika kuhakikisha haki za wanawake kiuchumi,
kijamii, na kisiasa zinapatikana na zinalidwa.
Aidha, kuadhimisha Siku ya Wanawake Duniani ni kuhamasisha
jamii kuhusu umuhimu wa kutambua na kuthamini uwezo na mchango mkubwa wa
wanawake katika kuleta maendeleo, kuelezea jitihada mbalimbali zilizofanywa na
Serikali na wadau wengine katika kuwajengea uwezo wa kiuchumi na kijamii ili
waweze kushiriki kikamilifu kujiletea maendeleo yao, familia zao na Taifa kwa
ujumla.
Tanzania
ilianza kuadhimisha Siku ya Wanawake Duniani mwaka 1996, maadhimisho yamekuwa
yakiandaliwa Kitaifa na katika ngazi ya mkoa.
Hivyo maadhimisho ya mwaka huu 2016 “50 – 50 Ifikapo
2030; Tuongeze Jitihada”, ambapo Kauli mbiu hii inasisitiza kuwa na
mikakati thabiti yenye mwelekeo wa kufikia Agenda ya 2030 yenye malengo ya
kufikia asilimia 50 kwa 50 ya ushiriki wa wanawake na wasichana katika nyanja
zote za maendeleo.
0 comments:
Post a Comment