Wema
Sepetu ni mwanamke maarufu si Tanzania tu bali Afrika Mashariki na ana
mashabiki wengi zaidi – TeamWema. Tangu awe Miss Tanzania mwaka 2006,
mrembo huyu ameendelea kuwa kwenye headlines bila kupunguza.
Umaarufu
wake ulichangiwa zaidi na mahusiano yake ya kimapenzi na watu maarufu
kuanzia TID, Mr Blue, marehemu Steven Kanumba, Diamond na hivi karibuni,
mshindi wa BBA 2014, Idris Sultan. Lakini niseme kuwa uhusiano wake na
Diamond ndiyo uliomulikwa zaidi kuliko mwingine wowote.
Ni
katika uhusiano wao, jina la Diamond lilivuma zaidi hasa kwakuwa
kipindi wanaanza, Wema alikuwa tayari kwenye kilele cha umaarufu, na
hitmaker huyo alikuwa ameanza kuikwea ngazi.
Kwa
kipindi chote hicho, Wema amekuwa ni brand kubwa. Wema ni mgodi
unaotembea. Hii ni kwasababu hakuna staa mwingine wa kike Afrika
Mashariki mwenye kundi kubwa zaidi la mashabiki nyuma yake. Ni kundi
kubwa ambalo lipo tayari kumtetea na kumpigania katika nyakati zote,
mbaya au nzuri.
Kundi
hili limeendelea kuwa aminifu kwake hata pale anapoanzisha uhusiano na
mtu mwingine. Lilikuwa nyuma yake kipindi yupo na Diamond na hadi
walipoachana. Limeendelea kumfuata kipindi ameanzisha uhusiano na Idris
kiasi cha kuifanya couple hiyo itengeneze headlines nyingi ndani ya
muda mfupi.
Kwahiyo
kwa namna yoyote ile, Wema ni brand inayoweza kuingiza fedha nyingi.
Japo alitakiwa kuwa mbali sana kutokana na ushawishi alionao, nafurahi
kuona kwamba tayari ameigundua thamani yake na kuanza kuitumia. Napenda
kumuona Wema huyu wa sasa ambaye akili yake imefocus zaidi kibiashara na
kupush brand yake ya lipstick, Kiss by Wema Sepetu.
Napenda
ninavyoona anavyotumia nguvu kuisambaza na kutafuta mawakala nchi
nzima. Ninachofurahia zaidi ni kuona kuwa anaisambaza hadi Kenya ambako
kuna mashabiki wake wengi sana. Lipstick zake zipo katika rangi
mbalimbali na kwa muonekano wa picha ninazoziona, zinaonekana ziko poa.
Cha
msingi sana mashabiki wake wa kike na hata wanawake wengine tu
wanaopenda urembo, wamuunge mkono kwa kununua bidhaa za mzawa. Ni kwa
kufanya hivyo ndivyo tunavyoweza kutengeneza mastaa ambao hawaiishi kuwa
na majina tu, bali pia wanakuwa na uwezo kifedha. Naamini huu ni mwanzo
wa Wema kuliwekea thamani jina lake na kutengeneza bidhaa nyingi zaidi
sababu wateja wapo.
Leo
ameanza na lipstick, kesho anaweza kuja na perfume, lotion, mafuta na
bidhaa zingine kibao. Cha msingi napenda kuona akiendelea na mzuka huu
wa kupush brand yake yeye mwenyewe kwa nguvu zote. Ni hivi ndivyo
wanavyofanya mastaa wa nje kama akina Diddy kupromote bidhaa zao.
Kwa
kufanya hivi na kwa jitihada zake, haitachukua muda mrefu kampuni kubwa
kuonesha interest ya kuwekeza mabilioni ya shilingi kwenye brand yake.
Huyu ndiye Wema tunayempenda, na sio yule wa drama ambaye mwisho wa siku
tumejikuta tukimpa jina The Drama Queen.

0 comments:
Post a Comment