Chama cha walimu wilayani Namtumbo mkoani Ruvuma kimeanza
safari ya kutoa semina kwa walimu wa kike wa wilaya hiyo kuhusiana na mambo
mbalimbali yanayohusu haki za wanawake
kulingana na katiba ya jamhuri ya muungano wa Tanzania.
Semina hiyo ilifanyika katika ukumbi wa halmashauri ya
wilaya ya Namtumbo ambapo katibu wa chama cha walimu wa wilaya ya Namtumbo Bi.Estha
Chabruma aliwasilisha mada mbili ambazo ni mada ya mirathi na mada ya
ujasiliamali kwa walimu wa kike.
Akielezea kuhusu mada ya mirathi katibu wa chama huyo
aliwataka walimu hao kuwa makini katika kuzijua sheria za mirathi kwa kuwa wanawake wengi ambao hawajui haki hizo
hunyanyaswa na kuhangaika na mzigo wa familia aliyoachiwa na marehemu mumewe
kutokana na kutopata hakistahiki za mirathi hiyo.
Aidha alitaja sheria
za mirathi kwa mujibu wa katiba ya jamuhuri ya muungano wa Tanzania kuwa
zipo tatu ambazo ni sheria ya mirathi ya kiserikali,sheria ya mirathi ya kimila
na sheria ya mirathi ya kiislamu.
Hata hivyo alifafanua sheria ya mirathi ya kiserikali ( Indian
succession Act 1865)ambapo mgawanyo wa mali unaenda kwa watoto wa marehemu
ambao wanapatiwa theluthi mbili ya mirathi yote na wajane au wagane watapata
theluthi ya miradhi yote na endapo hakuna watoto nusu ya mirathi watapewa
wajane na nusu inayobaki watapewa ndugu wa marehemu.
Lakini pia katika sheria ya mirathi ya kimila mgawanyo wa
mali za mirathi umewekwa katika madaraja ambapo daraja la kwanza ni mtoto wa kiume wa
kwanza kutoka nyumba ya kwanza na daraja la pili ni la watoto wa kiume
waliosalia na daraja la tatu ni la watoto wa kike ambao kwa sheria za kuanzia
mwaka 1999 watoto wa kike wametakiwa nao kupewa haki ya kurithi ardhi tofauti
na huko nyuma.
Sheria ya miradhi ya kiislamu inaruhusu wajane kurithi moja
ya nane ya mirathi yote kama wanawatoto na watalazimika kuchukua robo ya mirathi kama
mjane hakubahatika kupata mtoto na mali inayobaki hugawanywa katika mafungu
matatu yaani theluthi mbili huchukuliwa na watoto wa kiume na theluthi
huchukuliwa na watoto wa kike .
Mada nyingine iliyotolewa katika semina hiyo ilikuwa ya
ujasiliamali ambapo walimu hao waliambiwa kuanza kujishugulisha na kuacha kuwa
tegemezi hasa kwa kuanza kidogo kidogo
kujifanyia biashara na mwishowe kuondokana na utegemezi.
Mwalimu Fatuma Hassani akichangia mada ya ujasiliamali alisema
kuwa walimu wengi wanapenda kujikwamua katika maisha lakini kinachowabana ni
muda kwani kuanzisha biashara ni swala dogo lakini biashara inahitaji muda wa
kutosha wa kusimamia ambapo wao muda rafiki kwao ni siku ya jumamosi na
jumapili pekee.
itakavyoruhusu. Na Yeremias Ngerangera
0 comments:
Post a Comment