Takriban
watu 12 wameuaua katikamapigano yaliyotokea katika vijiji ndani ya
Jamhuri ya Afrika ya kati. Huu ni uvamizi wa kwanza na mauaji tangu
Faustin-Archchange Touadera kuchaguliwa kama rais mapema wiki jana.
Mashambulizi
hayo yalifanyika karibu na mji wa Bambari ulioko maeneo ya kati ya
Jamhuri ya Afrika ya kati. Maafa hayo yalisababishwa na wizi wa mifugo
au mapigano ya kikabila la fulani. Maafisa
wa serikali walisema hakuna dalili inayoonyesha kwamba mapigano hayo
yalisababishwa moja kwa moja na uhasama wa wa kisiasa, kijamii na
kidini.
Mapigano baina ya makundi yanayounga pande hasimu za
kisiasa yamesababisha vifo vya maelfu ya watu huku wengine wengi
wakiwachwa bila makao tangu mapigano yazuke mwaka wa 2013.
Katika
uvamizi huu wa hivi karibuni, maafisa wa serikali waliambia shirika la
habari la Reuters kwamba watu 6 waliuaua kwenye vijiji tofauti siku ya
jumamosi. Diwani wa sehemu hiyo na kiongozi mmoja wa kundi la
vijana katika eneo hilo waliambia Reuters kwamba wanawake watatu kutoka
jamii moja walichinjwa kutoka umbali wa kilomita sita karibu na mji wa
Amassaka Topi.
Mahakama
ya kikatiba iliidhinisha ushindi wa
aliyekuwa profesa wa hesabu Faustin-Archange Touadera siku ya jumanne
baada ya awamu ya pili ya uchaguzi mnamo Februari 14, na kupeana mwanga
wa kuapishwa kwake tarehe 25 mwezi huu. Touadera ameahidi kutoa kipao
mbele kwa urejeshwaji wa amani na kuwanyang'anya silaha makundi ya
wanamgambo.
Mji
wa Bambari umekumbwa na mashambulizi ya mara kwa mara mwaka jana licha
ya kuwepo vikosi vya umoja wa mataifa vya kulinda amani.
kwa hisani ya Ruvuma news
0 comments:
Post a Comment