WAZAZI wa vijiji vya Kata ya Barai iliyoko Wilayani Karatu Mkoani
Arusha wameiomba Serikali ya awamu yaa tano kuchunguza sababu za watoto
wao kufanya vibaya katika mitahani ya kuhitimu darasa la saba.
Aidha
alibainisha kuwa mbali na tatizo la umbali mrefu pia wanafunzi wamkuwa
wakisumbuliwa na tatizo la njaa kwani shule hizo zimekuwa hasipikii
wanafunzi mashuleni mchana kutokana na kutokuwa na bajeti hiyo.
Kwa
upande wake mmoja wanafunzi hao ambao alijitambulisha kwa jina la
Gilony Gitonyi alisema kuwa wamekuwa wanashindwa kusoma kutokana na njaa
pamoja na kukosa mda wa kujisomea pindi wanaporudi nyumbani kwani muda
mwingi wamekuwa wakiutumia kwa ajili kuchunga mifugo pindi wanaporudi
majumbani.
Akizungumzia
swala hilo mbunge wa jimbo la karatu Willy Qambalo alisema kuwa kwa
upande wake anaona suluhisho la kutatua tatizo hilo ni pamoja na
kujenga mabweni ilikuweza kuwasadia wanafunzi kupata elimu ili kila
mwanafunzi asome apoapo shuleni ili kuweza kujipatia muda wa kujisomea.
"unajua kujengwa kwa haya mabweni
pia itasiadia kuwapata wanafunzi kirahisi ambao muda wamekuwa wakiacha
masomo na kwenda kuchunga mifugo jambo ambalo linapingwa vikali na
wazazi wa vijiji hivyo na pia wanafunzi hao watapata muda mrefu wa
kujisomea na swala wao kupata njaa litapungua kwani kutakuwa na chakula
shuleni kwa ajili yao"alisema Qakambalo
Aidha
Tafiti zinaonyesha walimu ,wenye utovu wa nidhamu watoro na walevi
katika maeneo ya mijini ndio hupelekwa katika shule hizzo zilizoko
maeneo ya porini kama adhabu kwao.Swali la kujiuliza je mwalimu huyu
atakuwa na nia ya kuwafundisha wanafunzi?Kupelekwa kwa mwalimu huyu kama
adhabu badala ya eyey kuridhia Kujua kusomaa na kandika kwa wanafunzi
hawa itakuwa ni ndoto.
Na Woinde Shizza,Karatu.
0 comments:
Post a Comment