Habari Mpya

Tuesday, May 31, 2016

Papa -Waajiri wasiolipa mishahara ya haki wafanyakazi wao ni wenye dhambi kubwa.

Baba Mtakatifu Francisko ameonya waajiri wanaopenda kulipa ujira mdogo  wafanyakazi wao kwa makusudi ya kujilimbikizia utajiri.



Papa ametoa onyo hilo, wakati wa Ibada iliyofanyika Kanisa dogo la Mtakatifu Marta mesema kufikia hatua hiyi ni dhuluma , ni kunyonya nguvu wafanyakazi. Matajiri hao ni makupe wanyonya damu na wanatenda dhambi ya mauti. 

Ameelezea hayo wakati  akitafakari somo la kwanza la siku,  aya kutoka  Barua ya Mtume Yakobo , ambamo  anatoa onyo kali kwa matajiri bahili wanaojilimbikiza mali kwa kunyonya nguvu za wafanyakazi wao.
Method Charles
Baba Mtakatifu
Amesema si vibaya kuwa mtu   tajiri , lakini mapato  yanayoleta utajiri huo yawe ya haki, na isitokane na kugandamiza wafanyakazi wanaoleta utajiri huo. 

Papa amehimiza kile kinachoitwa “teolojia ya mafanikio”, kwa mujibu wa sheria ya Mungu inayotaka utendaji wa haki , katika kupata utajiri. 

Papa amesisitiza kwamba, tatizo hasa,  ni vigumu  kumtumikia Mungu na mali. Ameutaja daima moyo wenye  kushikamana na fedha na  utajiri , huondoa  kirahisi, kiungo katika mnyororo  wa uhuru wa kumfuata Yesu. 

Mtume Yakobo katika waraka wake ameonya waajiri  watoa malipo ya haki kwa wafanyakazi wao , kwa kuwa  iwapo watawapujwa kilio chao kitafika katika masikio ya Bwana wa haki.  
Hata hivyo Papa alieleza na kuongeza kukemea kwamba,  utajri  unazalishwa kwa kuwanyonya wengine , unyonyaji  huo husababisha umaskini na hivyo ajira hiyo inakuwa haina tofauti na utumwa.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

0 comments:

Item Reviewed: Papa -Waajiri wasiolipa mishahara ya haki wafanyakazi wao ni wenye dhambi kubwa. Description: Rating: 5 Reviewed By: mcjohnminja.blogspot.com
Scroll to Top