Habari Mpya

Monday, June 20, 2016

Benny Hinny na Pastor Chriss Kuhudumu pamoja Jijini Lagos

Haijawahi tokea kuweza kuwakutanisha watumishi wa Mungu wawili nguli duniani Pastor Chriss Oyakhilome na Pastor Benny Hinn pamoja katika madhabahu moja.

Wahubiri hao maarufu ijumaa ya tarehe 28 na 29 October 2016 wanatarajia kuendesha ibada kubwa tatu zilizopewa jina “MIRACLE HEALINGS AND IMPARTATION SERVICES” katika kanisa la Christ Embassy’s Loveworld Convocation Arena, lililoko Ikeja jijini Lagos nchini Nigeria.Pastor Chriss Oyakhilome ndiye muasisi wa makanisa ya Christ Embassy duniani.

Nchini Nigeria Kwa miongo kadhaa sasa haijawahi tokea muhubiri yeyote kutoka nje ya kanisa la Christ Embassy kupata nafasi ya kuhudumu katika mimbari ya kanisa hilo, kwa ujio wa Benny Hinn ndani ya Christ Embassy kunakwenda kutengua historia hiyo.

Habari ya wawili hao kuhudumu pamoja imepatikana kwenye website ya Benny Hinn.Hakika hii itakuwa ni habari njema kwa kanisa duniani ambapo wahubiri wakubwa wakionyesha umoja wa kristo katika huduma.
BeKgy8ICcAAjwL8
Pastor Chriss akiwa kwenye Kongamano la Maombi nchini India Mwaka 2014

Mwaka 2014 wawili hao kwa pamoja walipangwa kuhudumu katika kongamano la Maombi nchini India katika jiji la Bangalore, ni pastor Chriss pekee aliyeweza kufanya hivyo huku Benn Hinny alikosa kuhudumu.

Kulikuwa na taarifa zisizo rasmi kuwa kutokufika kwa Benny Hinn katika kongamano hilo kutokana na tatizo la viza yake kulitokana na shinikizo la utawala wa dini ya Kihundu yenye wafuasi wengi nchini humo.Kufika kwa Benny Hinny nchini umo kulitafsiriwa kungepelekea idadi kubwa ya watu kujiunga na ukristo.

  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

0 comments:

Item Reviewed: Benny Hinny na Pastor Chriss Kuhudumu pamoja Jijini Lagos Description: Rating: 5 Reviewed By: mcjohnminja.blogspot.com
Scroll to Top