Habari Mpya

Thursday, June 09, 2016

Kodi ya Kusajili Gari Kwa Kuandika Jina Lako Yaongezeka Kutoka Milioni 5 Hadi 10

Bajeti ya Serikali iliyotangazwa huenda ikapunguza idadi ya watu wanaopenda kuonekana tofauti, kwenye usajili wa magari kwa kuandika majina yao badala ya namba.

Wamiliki wa magari wanaotaka kusajili namba binafsi kama kuweka majina yao, sasa watalipa Sh10 milioni badala Sh5 milioni za awali, kwa kipindi cha miaka mitatu.

Akitoa mapendekezo ya mapato na matumizi ya Serikali kwa mwaka 2016/17 jana, Waziri wa Fedha na Mipango, Dk Philip Mpango aliomba Bunge liridhie kufanya marekebisho ya Sheria ya Magari (Kodi na uhamisho wa umiliki) ili kupandisha usajili wa namba hizo.

Namba hizo binafsi zilizoanzishwa miaka minne iliyopita, zinaruhusu mtumiaji kuandika jina au neno lolote kwenye gari lake tofauti na namba za kawaida zinazotumika nchini.

  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

0 comments:

Item Reviewed: Kodi ya Kusajili Gari Kwa Kuandika Jina Lako Yaongezeka Kutoka Milioni 5 Hadi 10 Description: Rating: 5 Reviewed By: mcjohnminja.blogspot.com
Scroll to Top