PETER Kibatala wakili wa Josephati Gwajima Askofu wa Kanisa la ufufuo na uzima jana aliiomba mahakama kuahirisha tarehe ya kusikiliza kesi inayomkabili askofu huyo sababu anaumwa.
Kibatala alidai mahakamani Kisutu kuwa kutotokea kwa mteja wake jana kulitokana na yeye kuwa nje ya nchi kwa ajili ya matibabu.
Wakili huyo aliwasilisha madai hayo jana
katika Mahakaama ya Hakimu Mkazi Kisutu mbele ya Hakimu Syprian Mkeha
Hakimu Mfawidhi anayesikiliza kesi hiyo inayomkabili Gwajima
Mahakama ilikubali ombi hilo na kwamba kesi hiyo itatajwa tena 2 Agosti mwaka huu.
Katika
kesi hiyo Gwajima anadaiwa kutoa lugha ya matusi dhidi ya Mwadhama
Polycarp Kardinali Pengo, Askofu wa Mkuu wa Kanisa Katoliki Jimbo la Dar
es Salaam.
Gwajima
anadaiwa kufanya tukio hilo kati ya 16 na 25 Machi, mwaka 2015 katika
Viwanja vya Tanganyika Packers Wilaya ya Kinondoni, Dar es Salaam.
0 comments:
Post a Comment