Habari Mpya

Tuesday, July 26, 2016

Haya ni manufaa ya kula nanasi kila siku…

pineapple_1_1_1_1

Moja kati ya matunda ambayo yanapendwa zaidi ni tunda la nanasi, linapendwa zaidi kutokana na ladha nzuri na tamu ambayo inatokana na sukari iliyoko ndani ya tunda hili ambapo inafanya tunda hili kuwa moja kati ya matunda ambayo yanatumika sana kwa kutengeneza juice.
Hata hivyo baada ya kusoma taarifa hii ya utafiti utapata sababu zaidi za kupenda kula mananasi, zipo faida nyingi sana kwenye mwili wa mwanadamu faida ambazo ni za kiafya zaidi.

Mananasi yana virutubisho hivi muhimu kwa mwili wa mwanadamu.
Mananasi ni chanzo muhimu sana cha vitamin pamoja na madini ambayo yanasaidia kuimarisha afya ya mwanadamu ambazo ni kama vile Thiamin, Riboflavin, Vitamini B-6 , Folate , Acid ya Pantothetic pamoja na madini ya Magnesium, manganese na potasia.
Katika hesabu za kitabibu, kipande kimoja cha nanasi kinatosha kuongeza 131% ya vitamin c ambayo mwili wako unaihitaji kwa siku moja.
pineapple1

Mananasi husaidia kutibu vidonda na uvimbe.
Moja kati ya vurutubisho vilivyoko ndani ya nanasi kinaitwa Bromelain, husaidia sana kuondoa maumivu kwenye viungo, kupunguza hali ya uvimbe kwenye tezi  na hata kupunguza uvimbe wa kawaida ambao umetokea ndani ya mwili na pia humsaidia sana mtu akiwa amefanyiwa upasuaji.

Mananasi husaidia Mfumo wa usagaji (Mmeng’enyo) wa chakula.
Manansi yana virutubisho vya kambakamba (fibre) ambavyo husaidia sana kwenye kusagwa kwa chakula mwilini, kirutubisho cha Bromelain pia husaidia kwneye kusaga chakula tumboni kwa kusaidia kuvunja vile vipande vya protini.

Manufaa ya nanasi kwenye ngozi
Vitamini C ipatikanayo kwenye mananasi husaidia sana kuipa ngozi mng’ao ambao unahitajika, mishipa midogo ya damu pia hufaidika sana kutokana na mananasi pamoja na viungo vingine vya mwili na mifupa pia.

Manufaa ya nanasi kwenye mifupa
Mananasi yana madini aina ya Manganese ambayo husaidia kuzalisha nishati mwilini huku ikisaidia kutoa ulinzi kwa seli za mwili wa mwanadamu.
Madini haya yanasaidia sana ufanyaji kazi wa madini mengine na virutbisho kama Thiamine na Biotin ambayo kazi yake kubwa ni kusaidia kufanya mifupa kuwa migumu na yenye afya zaidi na pia husaidia kuyayusha vyakula vyenye mafuta.

Mananasi husaidia Macho .
Tunda aina ya nanasi lina vitamin A pamoja jna kirutubisho aina ya Beta-Carotene ambavyo kwa pamoja husaidia mfumo wa kinga ya mwili na afya ya macho.

Mananasi hutoa nguvu na nishati na kushusha shinikizo la damu.
Mananasi ya kiwango kikubwa cha Vitamini B1 na B6 ambavyo ni vyanzo muhimu sana vya nishati pamoja na kuvunjavunja sukari kwenye mfumo wa usagaji wa chakula.
Madini ya shaba pia yanapatikana kwenye mananasi yanasaidia sana kutoa afya kwa seli nyekundu zinazosaidia kutengeneza damu na madini ya potasia ambayo yanasaidia kuweka mapigo ya moyo sawa na kushusha shinikizo la damu.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

0 comments:

Item Reviewed: Haya ni manufaa ya kula nanasi kila siku… Description: Rating: 5 Reviewed By: mcjohnminja.blogspot.com
Scroll to Top