NANI MJINGA NA NANI MJANJA KATI YA HAWA????
Siku moja nilikutana na kihoja kimoja ikanibidi nichekee kimoyoni ili mtu yeyote asijekujua kama ninacheka coz ningezua balaa…
Kuna familia ilikuwa inajishughulisha na ufugaji wa kuku, na palikuwa na kijana aliyekuwa anawasimamia wale kuku kwa bidii zote, kwa kuwapa chakula, maji na walipokuwa wakiumwa anwapa dawa wanapona!
Sasa siku niliyoingia kwenye hiyo familia nilikutana na hichi kijihoja, siku hiyo walichinja kuku, na huyo kuku akagawanywa mara nne, miguu ikiwa imetolewa pamoja na kichwa cha huyo kuku, ijapokuwa nayo pia ilipikwa, sasa tulipofika mezani kabla ya kula nikafanyiwa utambulisho kwa ufupi, na kwa yule kijana msimamizi wa kuku, na kuambiwa ndiye mtoto wao wa kwanza wakiume, na alikuwa na mdogo wake aliyemfuata.
Sasa mama akawapakulia watoto chakula sahani moja akaweka ile miguu 2 na kile kichwa, na sahani nyingine akaweka upande mmoja wa kuku kati ya ile minne, akawaita watoto waje wachukue chakula, akaja mdogo akapewa ile yenye miguu na kichwa, alipofika mkubwa kuona sahani yake ina nyama moja akachukia nakuanza kulaum huku akisema sikubali, sikubali, yaani miee nilishe niwatunze alafu nile nyama moja??? Nasema sikubali!!! Ikabidi aulizwe unatakaje????
Ndipo aliponishangaza kwa kusema anataka ile sahani aliyopewa mdogo wake apewe yeyee…. Wote tukapigwa na butwa!!!! Ikabidi mdogo wake achukue ile nyingine na kaka yake apewe ile aliyoing’ang’ania yenye miguu na kichwa kisa ina wingi kiidadi…
Sasa mie baada yakutoka pale nikaanza kujiuliza ule ni ujinga wa kiasi gain?? Kiasi cha mtu kuacha bonge la paja na kulilia miguu na kichwa, nikiwa naendelea kufikiri nikajikuta nimefika katika serikali yetu,
Nikaona vile tunavyong’ania miguu ya kuku na vichwa vyaake, na kuwaachia wasiousika minofu yote wanaondoka nayo, wakati sisi ndiyo tuliofuga, na kuwahangaikia, alafutwaambulia miguu na vichwa! Tunabakia kujisifia ati siye ni wafugaji wazuri na tunaongoza kwa kuwa na kuku wengi sanaaaa….. sasa faida yake nini kwetu wakati kuku akichinjwa tunaishia kula miguu????
Nahisi wengi bado hawajanielewa ninachozungumzia… ngoja niwafungue kidogo…
Tukija kwa TANZANITE yenyewe inatokea hapa TZ lakini soko kubwa liko KENYA na INDIA , wao ndiyo wanafaidi mibonge ya minofu ya vile tunavyovifuga!!!! Tunaishia kutunza milima ya migodi, alafu ikichimbwa mawe makubwa yanasafirishwa na ndege kwenda nje nchi, siye twaachiwa michangamichanga!!!
Mengineyo unayajua wewe,
na usijidanganye kwa kula miguu ya kuku ukaona wewe mjanja umekula nyama nyiiiiiiingi.. wajanja ni wale wanaokula minofu na hawajaiangaikia hata kiduchu…..
Tunaombeni rasilimali zetu zitufaidishe kwa sisi wananchi wa hapa Tanzania , kwa kuboresha sekta muhimu katika jamii kama ELIMU, MATIBABU, CHAKULA, na UCHUMI kwa ujumla, kisha zinazobakia ndiyo zitoke nje.
I LOVE MY COUNTRY TANZANIA !!!!!!
0 comments:
Post a Comment