Matokeo ya kidato cha 4 yalipotoka kati ya wanafunzi waliofeli kuna
waliojiua. Kwa taarifa nilizonazo ni kuwa wanafunzi 4 waliripotiwa na
vyombo vya habari kuwa walijiua! Pia kuna wale waliochanganyikiwa
kisaikolojia ambao nadhani ni wengi sana japo hawajaripotiwa kwenye
vyombo vya habari.
Wiki iliyopita serikali ikasema kuwa kulifanyika
makosa katika kupanga matokeo (grading) na ndio sababu KUBWA ya kufeli.
Kwa hiyo re-grading and standardization inabidi vifanyike kwa kutumia
mfumo uliotumika 2011 na sio mfumo mpya.
Sasa maswali yangu ni:-
1. Hao waliojiua matokeo yao yakirekebishwa na wakaonekana wamefaulu
itakuwaje? Watafufuliwa ili waendelee na shule form 5 na 6?
2. Je kuna kitu kitafanyika kuwatibu wale waliopata matatizo ya kisaikolojia?
3. Je tuna uhakika gani kuwa mfumo uliotumika kupanga matokeo ni mpya
na sio wa 2011? kama ni mpya ni sababu zipi zilipelekea kutumika kwa
mfumo huo? Nani walioidhinisha? Na je katika kuruhusu matokeo yatangazwe
ofisi husuka za serikali (Wizara ya Elimu, Baraza la mitihani na ile
ofisi ya rais na waziri mkuu) zilliridhia matokeo yatangazwe? Na kama
zilidhiria je ina maana kwa kukubali yarudiwe watakuwa wanakubali kula
matapishi yao wenyewe?
4. Ni kwanini kumekuwa na ukimya mkubwa sana kutoka ofisi hizo tajwa hapo juu, mara tu baada ya kutoa tamko la kurudiwa?
Ni mawazo ya haraka haraka kichwani mwangu!!
according to Brother Chris
0 comments:
Post a Comment