Wajaleo waondoka leo, ni msemo
wa watu wa mkoa wa Tanga, ila msemo
huu huendana na mazingira yenyewe
kutokana na ukarimu
waliokuwa nao watu waishio
mkoa huo, ama
kwa hakika ukisikia
mkoa wa Tanga utaamani
angalau siku mmoja
upotee njia ukajionee
mwenyewe, kwani mji
wa Tanga ni
mji ambao sio
mdogo sana wala
siyo mkubwa, bali ulijipatia
umaarufu hivi karibuni
kutokana na baadhi
ya maeneo kuwa
kama sehemu za vivutio
kwa wageni na
hata wenyeji waishio
nje na ndani
ya mji huo.
Mkoa wa
Tanga umegawanyika katika
Wilaya saba ambazo
ni Handeni , Lushoto, Kilindi, Korogwe, Pangani,
Muheza na Tanga
yenyewe bali katika
wilaya hizo ni
Wilaya ya Tanga
ambayo ndiyo wilaya
iliyobeba jumla ya wilaya
zote yenye vivutio vya kitakii na vya
kiasili.
Tukiangalia katika Wilaya
hii kunabadhi ya maeneo
yamekuwa vivutio vya
asili kwa wageni
na hata kwa baadhi
ya awatalii wandani ya mkoa
huo wa Tanga, kwani
mapango ya amboni
yamekuwa kivutio kikuu cha asili,
pia tukiangalia hata katika mbuga za wanyama iliyoko
mkoani humo ambayo
inajulikana kama Sadani,
japo leo nazungumzia mapango
ya asili ya
amboni.
Mapango ya
amboni ni mapango ya asili kwa maana siyo ya mapango yaliyo
tengenezwa na binadamu,
bali mapango haya
ni matokeo ya
mmomonyoko wa miamba ya chokaa ambayo ni mabadiliko ya carboni na tukiangalia
kwa haraka tunaona kuwa
kunamgawanjiko wa vitu kumi na tatu na kuanza kuelezea
kimoja baada ya
kingine na kueleza kama
kinatumika au kilitumika vipi
hapo kale na hata sasa
kinatumikaje.
Mapango haya
yalianza shughuli zake za utalii mnamo
mwaka 1980 na 1990 kuanzia hapo wenyeji
wa mkoa huo walikuwa wanatembelea
mapango hayo bila ya malipo yoyote na
mnamo mwaka 1999 ndipo walianza
kufanya malipo katika mapango haya
kutokana na baadhi ya wenyeji
waishio karibu na mapango
hayo kuanza kutembelea
bila utaratibu maalum ndipo
walipoanza utaratibu wa
kulipia ili kuweka mazingira ya mapango
haya katika hali ya usafi.
Tukianza na
kituo cha kwanza katika mapango haya ni kituo cha mzimu wa mababu ambao
mnamo karne ya 16 wananchi waishio
katika mazingira hayo walitumia sehemu hiyo kufanyia ibada na matambiko katika
sehemu hiyo na kwa sasa wanaitumia sehemu hiyo kama sehemu ya kufanyia
matambiko hata kwa wageni wanaoingia nchini kwa lengo la kutalii na huitumia
sehemu hiyo kama mmojawapo yakuomba kwa imani na kufanikiwa kwa walio wengi.
Kundi
lingine katika mapango hayo ni kituo ambacho hutumiwa kama maficho ya watu
wawili ambao walipotea katika mapango hayo mmoja akiitwa Osale Otango na wa
pili ni Paulo Hamisi hao watu walikuwa wanadaiwa kufanya fujo katika jamii na
kuwapora wanaoingia ndani ya mapango na mara wafanyapo matukio hayo hukimbia
katika mafichoyao, na watu hao waliishi zaidi ya miaka minne ndipo wanajamii
walipo anza kuwatafuta na mbali yahayo yote watu hao bado wanakumbukwa kwa kile
walicho kuwa wanakifanya katika mapango hayo mnamo mwaka 1950.
Vilevile
watu hao walikuwa wafanya yote hayo kutokana na taratibu ambazo waklikuwa
hawakubaliani nazo ambazo walikuwa wafanyiwa na walowezi ndipo walipoamua
kufanya fujo na kuwavamia walowezi hao.
Hata
hivyo kuna kunfi la nne ambalo simulizi zilidai kuwa mnamo mwaka 1941 wazungu
waliingi na mbwa waliingia ndani ya mapango na kupotea japo hazikuishia hapo
simulizi zilidai kuwa wazungu hao hawakutaka kuingia na mwenyeji na matokeo hao
walipotea katika pango na pia inasemekana kuwa wenyeji wao walipofuatilia
walikuta miguu ikielekea shimoni pia kwa simulizi hizi ziliendelea kuwa baada
ya mwezi mmoja na nusu mbwa alionekana
katoka mlima Kilimanjaro na huo ndio mwisho wa simulizi hizi.
Pia
mapango hayo yamekuwa ni urithi wa Taifa na urithi wa utamaduni kwani hata kwa
upande wa masomo kuna baadhi ya maeneo yamekuwa kama sehemu ya kujifunzia hasa
katika somo la jiografia kuna baadhi ya miamba inakuwa na tabia kujiunga kama
mvua ikinyesha miamba hiyo hutengeneza kitu kiitwacho stalactmait.
Mbali na
hayo tukiangalia mwisho wa Osale na Paulo umebaki kuwa historia kwani Paulo
alifia Lushoto ambapo alimbaka mwanamke mnamo mwaka 1957 kwakuwa watu hao
waliishi kwa miujiza na inasemekana kuwa mwnamke aliyebakwa na Paulo alipigwa
risasi upande wakushoto na kuaga dunia.
Hata kwa
upande wa Osale naye alifariki mnamo mwaka 1958
huko na kwa mujibu wasimulizi hazikuelezwa alipofia na kama aliumwa au
la,wote hao walizikwa huko Lushoto na huo ndio mwisho wa historia
yao.Kwakusimuliwa huwezi kuamini jinsi ambavyo mapango hayo yalivyo kuwa
kivutio kizuri kwa watilii wa nje ya nchi na hata kwa walio ndani ya
nchi.tembelea mapango yetu yaliyo ndani ya nchi nzuri yenye amani na utulivu
Tanzania.
0 comments:
Post a Comment