Habari Mpya

Saturday, August 24, 2013

MAPISHI MKATE WA NDIZI





   Kuna aina mbalimbali za mikate.Mara nyingi aina hutofautiana kutokana na viungo vinavyotumika kutengenezea.
   Katika mapishi leo hii nitakuelekeza namna ya kutengeneza mkate wa ndizi.kama nilivyokueleza hapo awali kwamba kuna tofauti kubwa baina ya mkate mmoja na mwingine.Jambo linalosababishwa na kuwepo kwa viungo tofauti.
   Mkate wa ndizi umekuwa na tofauti kubwa ya ladha ukilinganisha na mikate mingine , hasa kwa vile ina viungo tofauti na mikate ya kawaida.
   Pamoja na kuwa aina hii ya mikate imekuwa ukifahamika sana katika maeneo yanayolima zao la ndizi.Bado imekuwa ni kazi kubwa kutengeneza.
   Kwa kawaida vipimo vya upishi huu hutegemea zaidi na idadi ya walaji ulionao.

Mahitaji
Sukari kikombe kimoja
Siagi theluthi kikombe
Mayai mawili
 










Ndizi mbivu zilizomenywa na kusagwa kikombe kimoja na nusu
Maji theluthi kikombe
Unga wa ngano kikombe kimoja nanusu cha chai
Unga wa soda kijiko kimoja cha chai
Chumvi kijiko kimoja cha chai
Baking poda robo kijiko cha chai
Karanga nusu kikombe cha chai

Namna ya kupika
   Changanya sukari na siagi kwenye bakuli moja kubwa la udongo ama plastiki, hakikisha vinachanganyika kabisa, kasha weak mayai na endelea kukoroga (hakikisha unakoroga kwa kuzungusha upande mmoja tu), halafu weka unga wa ngano.
   Vikishalainika weak ndizi na saga kwa muda wa dakika tano. Ikiwa unatumia mashine ya kusagia sekunde thelathini tu zinatosha.
   Chukua viungo vingine vyote vilivyobaki isipokuwa karanga na kasha weka kwenye mchanganyiko wako. Changanya hadi vichanganyike vizuri na kasha waweza weka karanga endapo utapenda.
   Acha mchanganyiko wako uumuke kwa muda wa dakika 30.Baada ya hapo mimina katika bati la kuokea tayari kwa kuoka.Okoa kwa muda wa dakika 30 hadi uwe umeiva kabisa.
   Baada ya hapo ondoa weka pembeni, acha upoe.Ukisha poa kabisa waweza kata mkate wako tayari kwa kula.
   Mkate huu unaweza kula na chai ya maziwa ama kinywaji chochote kisichokuwa na kilevi.

Na; Maria Mtaita      
 
      
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

0 comments:

Item Reviewed: MAPISHI MKATE WA NDIZI Description: Rating: 5 Reviewed By: mcjohnminja.blogspot.com
Scroll to Top