Karibu mpenzi msomaji wa safu hii ya urembo na mitindo
.Bila shaka unaendelea vizuri na shughuli za hapa na pale. Msomaji wangu kama
ilivyo ada ya safu hii huwa tunazungumzia masuula ya mitindo na urembo na siku
ya leo tutaongelea kuhusu uvaaji wa
magauni marefu. Vazi hili linaweza kuwa katika mfumo wa khanga , kitenge ,na
pia linaweza kuwa katika vitambaa vya aina tofauti tofauti kama vile vitambaa
vya kisukari, tetroni na vile vya mpira.
Vazi hili linaweza
kutengenezwa na kitambaa kilichorembwa na maua. Rangi ni miongoni mwa vitu
muhimu katika sualaa la urembo na mitindo, pia rangi imekuwa ikitumika
kutambulisha baadhi ya watu na maeneo yao
Katika vazi letu la
leo ambalo ni gauni, rangi ni kitu cha
kuzingatia ili kuweka muonekano mzuri pindi uvaapo gauni lako .Kwa mujibu wa
wataalamu wa urembo na mitindo, miongoni mwa rangi zinazo onekana kupendwa na kutawala
katika mitindo ya gauni ni zile za asili
kama vile kijivu, bluu, manjano, maziwa, nyeusi, kijani, nyeupe, waridi na
nyekundu .Rangi hizo zimeonekana kupendwa sana kutokana na sifa yake ya
kuonekana zaidi.
Uvaaji wa vazi hili
unaweeza ukavaa na viatu vya wazi (open
shoes), viatu vya kuziba kote(simple
shoes), au viatu virefu(high hills), hapo ni kwa upande wa viatu. Katika
kuongeza mvuto zaidi unaweza ukavaa na mkanda (belt) wa rangi yoyote ile na
ikavutia kwakuwa rangi zake huwa ni za asilia.
vaazi hili huwa
linapendeza kuendana na mwili wa mtu kwakuwa huwa ni marefu hadi chini na yanayoendana
na mwili wa mtu (kumshepu na kuvaa
kulingana na utamaduni na saizi ya mwili
wako.
Vazii hili linaweza
kuvaaliwa sehemu mbalimbali kama vile ofisini, sehemu za kuabudu, makazini, na
hata katika sherehe kwa kuwa humfanya mvaaji kuonekana mwenye mvuto ni
vizuri kuzingatia hali ya hewa, maadili na utamaduni wako.
0 comments:
Post a Comment