Habari Mpya

Tuesday, February 18, 2014

WALIJUA TENDE NA KAZI ZAKE WEYE....


Tende ni moja ya neema nyingi ambazo zimewekwa ktk ardhi hii kwa ajili yetu ili kunufaika kwayo. Tende ni mashuhuri sana kama chakula cha kawaida ktk nchi nyingi za Meditreniani. Qur’an tukufu inazitaja ktk aya nyingi kama vile (6:99, 16:67, 55:11) kama chakula kamili. Kwa vilie hata tende mija huleta mizania na chakula chenye afya.

1. Ina chakula aina ya wanga, nyama, mafuta na nyuzinyuzi za asili na aina nyingine nyingi za lishe, kama Chokaa, Salfa, Chuma, Potasium, Fosforasi, Magnesi, Shaba na Magnesium.

2.Tende zina athari ya Toniki kwa vile huyeyushwa kwa urahisi sana, hivyo hutumika katika kuleta nguvu kwa haraka.

3. Manufaa ya afya ni pamoja na kusaidia katika kupunguza uzito kwa vile ina mafuta kidogo, huzuiya upungufu wa damu kwa vile madini chuma ya kutosha, kinga ya Saratani kwa vile ina Magnesium.

4. Kuimarisha mifupa/meno kwaPotasiumu na Chokaa na Vitamini A+B.

5. husaidia nguvu ya macho kuona, Kusikia, Unyumbukaji wa ngozi(huzuiya ukaukaji wa ngozi, modomo, mpasuko wa kucha n.k).

6.Tende ni chanzo cha mara moja cha nishati na lishe, tende huchochea matokeo ya ufanyaji kazi, husaidia kutengeneza maziwa, hufudia upungufu uliojitokeza wa Madini chuma katika damu na kuongeza utengenezaji wa uboho(Bone marrow) wa mifupa ya mtoto mchanga. Na ndo maana Mtume(s.a.w) kaifanya kuwa ni Sunnah kwa mtoto aliyezaliwa kabla ya kupewa chochote basi atafuniwe Tende na kisha alambishwe majimaji yake. 


Na Abeid Ally

  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

0 comments:

Item Reviewed: WALIJUA TENDE NA KAZI ZAKE WEYE.... Description: Rating: 5 Reviewed By: mcjohnminja.blogspot.com
Scroll to Top