Mfuko wa Pensheni wa LAPF
pamoja na kutekeleza majukumu yake ya kila siku kwa mafanikio makubwa, bado
unafanya jitihada kubwa kuhakikisha kwamba huduma ya hifadhi ya jamii inamfikia
kila mtu bila kujali aina ya ajira yake. Kwa mazingira ya sasa ya sekta ya
Hifadhi ya Jamii, mtu yoyote mwenye shughuli za kuajiriwa au kujiajiri mwenyewe
anaweza kujiunga na Mfuko wa LAPF katika utaratibu wa kisheria au wa hiari.
Kama wahenga wasemavyo
maisha ni mipango, na hakuna aliyefanikiwa kimaisha na kudumu katika mafanikio
bila ya kuwa na mipango madhubuti pamoja na njia za kutekeleza mipango hiyo iwe
ya muda mfupi au mrefu.
Mfuko wa Pensheni LAPF ukiwa
na dira ya “kuwa Mfuko bora wa Pensheni
unaopendwa zaidi hapa nchini”,
umeweza kubuni utaratibu unaomwezesha mtu yeyote kujiunga na kujiwekea akiba
kwa lengo la kutimiza malengo mbalimbali ya maisha kupitia mpango wa LAPF-Uwekaji Akiba kwa Hiari au LAPF-Voluntary Savings Scheme (L-VSS).
Kupitia mpango huu, mwanachama aliyejiunga anaruhusiwa kujiwekea akiba
kulingana na kipato chake kwa wakati husika. Akiba inaweza kuwekwa kwa siku,
wiki, mwezi au msimu kulingana na kipato cha mwanachama. Kiwango cha uwekaji
akiba kinaweza kubadilika kulingana na hali halisi ya kipato.
Zifuatazo ni njia ambazo
mwanachama anaweza kutumia kufikisha akiba LAPF; kupitia ofisi za LAPF zilizopo
mikoa mbalimbali, benki (CRDB, NMB au NBC), Mitandao ya simu. Kila mwanachama
awekapo akiba na kufika LAPF mwanachama hujulishwa na kuthibitishiwa kuhusu
akiba yake. Pia kwa wanachama wenye uwezo wa kutumia mitandao wanaweza kuona
akiba zao kupitia tovuti ya Mfuko www.lapf.or.tz
Walengwa wa mpango huu ni
wale wote wenye uwezo wa kuzalisha kipato ikiwemo wakulima, wafanyabiashara,
wavuvi, madereva teksi, bajaji, bodaboda n.k. Pia wale ambao wameajiriwa katika
ajira rasmi na kuchangia kwenye Mifuko ya hifadhi ya jamii kwa utaratibu wa
kisheria wanahamasishwa kujiunga na utaratibu huu ili kujiweka katika mazingira
sahihi ya kustaafu kifahari.
LAPF inaamini mpango huu wa
ni kutimiza malengo na kujiwekea kinga
yatokeapo majanga yanayopelekea kusitisha uzalishaji kwa muda au moja kwa moja kwani
kwa atakayejiunga anaruhusiwa kuchukua mpaka asilimia 50, baada ya uwekaji wa
akiba kwa kipindi cha mwaka mmoja na kuendelea ili kutatua changamoto
mbalimbali ikiwepo kuboresha shughuli za kuzalisha kipato, pamoja na hayo pia
mpango huu hauna makato ya aina yoyote kwa mwanachama zaidi ya kujipatia faida
kila mwisho wa mwaka kutokana na mapato ya uwekezaji.
Uchangiaji wa hiari, unaweza
kufanyika kwa namna mbili. Mfumo wa akiba na ule wa bima.
Mfumo wa akiba mwanachama
anachangia kulingana na anavyopata na hivyo kustahili faida itokanayo na
uwekezaji. Wakati wa mwisho hulipwa mkupuo unaohusisha michango na faida
iliyopatika kutokana na mapato ya uwezaji kwa kipindi chote cha uanachama.
Mfumo wa bima kwa uchangiaji
wa hiari hufanywa kwa mwanachama kuahidi kujiwekea kiwango maalum kisichopungua
20% ya kima cha chini cha mshahara wa serikali kwa kipindi chote. Mwanachama
huyu akitimiza vigezo vya malipo ya uzeeni atalipwa kwa kanuni ya pensheni kama
ilivyo kwa wachangiaji wa kisheria.
Kwa mawasiliano zaidi;
E-mail: info@lapf.or.tz
Cell phone: 0784-648085
“STAAFU KWA UFAHARI NA LAPF”
0 comments:
Post a Comment