Habari Mpya

Thursday, December 04, 2014

DIAMOND PLATNUMZ AREKODI WIMBO NA JOYOUS CELEBRATION


Diamond (mwanamuzi maarufu TZ) akiwa na waimbaji mbalimbali, kwenye studio za SABC,  wakiwemo na waimbaji wa kundi la Joyous Celebration 
Mwimbaji wa muziki wa nje ya kanisa nchini Nasibu Abdul almaarufu kama Diamond Platnumz ni mmoja kati ya waimbaji wengine wengi wa Afrika walioshiriki pamoja na kundi maarufu la Joyous Celebration la nchini Afrika ya kusini kurekodi wimbo wa pamoja kupiga vita gonjwa la ebola, wimbo ambao ni wazo na utunzi wa Joyous Celebration.

Kazi ya kurekodi video wimbo huo imefanyika katika studio za shirika la utangazaji la Afrika ya kusini SABC nchini Afrika ya kusini huku umoja huo wa wasanii walioimba wimbo huo wakitumia jina la wimbo maarufu ulioimbwa na waimbaji nyota wa nchini Marekani kusaidia Afrika wa 'We are the world wenyewe wakiongeza neno Afrika mbele yake.

Ukiacha kundi la Joyous pia kulikuwa na waimbaji wengine kutoka Afrika ya kusini kama Mahottella Queens, Mafikizolo na wengineo pamoja na waimbaji kutoka Nigeria na pande nyingine za Afrika, Tanzania ikiwa imewakilishwa na mwimbaji huyo ambaye pia alijinyakulia tuzo tatu kati ya nne alizokuwa anawania zilizokuwa zimeandaliwa na kituo maarufu cha Channel O cha nchini humo. - See more at: http://www.gospelkitaa.co.tz/2014/12/diamond-platnumz-arekodi-wimbo-na.html#.dpuf
 
 
 






mwimbaji wa muziki wa nje ya injili nchi Tanzania Nasibu Abdul, almaarufu kwa jina la Diamond Platnumz, ni mmoja kati ya waimbaji wengine wengi wa Afrika, walioshiriki pamoja na kundi maarufu kwa nyimbo za injili nchini Afrika kusini Joyous Celebration, kurekodi wimbo wa pamoja kupiga vita gonjwa la EBOLA, wimbo huo ambao ni wazo na utunzi wa Joyous Celebration

kazi ya kurekodi video ya wimbo huo, imefanyika katika shirika la utangazaji la SABC, nchini Afrika kusini, huku umoja huo wa wasanii walioimba wakitumia jina la wimbo maarufu la wimbo ulioimbwa na waiimbaji nyota nchini marekani wa kusaidia bara la Afrika "WE 'RE THE WORLD" ila wao wakiongezea Afrika mbele yake.

ukiacha kundi la Joyous pia kulikuwa na kundi la waimbaji wengine toka Afrika kusini kama Mahottella Queens, Mafikizolo, pamoja na waimbaji wengine tokea Nigeria na pande nyingine za Afrika.

Tanzania ikiwa imewakilishwa na mwimbaji huyo ambaye amejinyakulia Tuzo tatu, kati ya nne, alizokuwa anawania ambazo ziliandaliwa na kituo maarufu cha Chanel O, huko nchi Afrika kusini


Baadhi ya waimbaji wa Joyous wakipata picha ya pamoja

Sylvester Funani wa Joyous, akiwa na waimbaji wa Mahottella Queens

  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

0 comments:

Item Reviewed: DIAMOND PLATNUMZ AREKODI WIMBO NA JOYOUS CELEBRATION Description: Rating: 5 Reviewed By: mcjohnminja.blogspot.com
Scroll to Top