Habari Mpya

Sunday, February 28, 2016

ASKARI WA KIKE AFYATULIWA RISASI MWILINI SIKU YAKE YA KWANZA KAZINI NA MWANAJESHI MLENGAJI WA SHABAHA.

Polisi mmoja wa kike nchini Marekani amepigwa risasi na kuuawa katika siku yake ya kwanza kazini.

Askari huyo bi Ashley Guindon alikula kiapo mapema siku hiyo hiyo kisha akaelekezwa na wakubwa wake kwenda nyumbani kwa mama mmoja kutatua mzozo wa kinyumbani katika kitongoji Washington, DC.

Bi Ashley akiandamana na wenzake wawili walikwenda Woodbridge, Virginia, kilomita 32 kusini mwa Washington lakini walipofika huko walifyatuliwa risasi kwa bahati mbaya Ashley hakubahatika.

Wenzake wawili pia walijeruhiwa vibaya na wamelazwa hospitalini.

Mshukiwa wa mauaji hayo ni mlengaji shabaha katika jeshi la Marekani aliwazidi maarifa maafisa hao wachanga.

Mwanjeshi huyo alikamatwa baadaye na vitengo maalum vya polisi.

Mwanjeshi huyo alikuwa amempiga risasi na kumuua mkewe papo hapo kabla ya Ashley na wenzake kutokea.
Hakukuwa na mtoto nyumbani wakati wa ufyatulianaji huo wa risasi.

Afisa mkuu wa kituo " Tunasikitika kuwatangazia kifo cha afisa wa polisi wa kituo cha Prince William County bi,Ashley Guindon, aliaga dunia kufuatia ufyatulianaji risasi katika mtaa wa Lashmere Ct akiwa kazini.

Mapema siku hiyo hiyo kituo hicho kilikuwa kimetoa picha ya afande huyo kwenye mtandao wa Twitter ikimkaribisha kwa huduma kwa wote.

''Tunafurahi kuwakaribisha afande Ashley Guindon na mwenzake kwa huduma kwa wote''BBC
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

0 comments:

Item Reviewed: ASKARI WA KIKE AFYATULIWA RISASI MWILINI SIKU YAKE YA KWANZA KAZINI NA MWANAJESHI MLENGAJI WA SHABAHA. Description: Rating: 5 Reviewed By: mcjohnminja.blogspot.com
Scroll to Top