Habari Mpya

Wednesday, February 24, 2016

FISI WASAKWA NA KIKOSI CHA KUZUIA UJANGILI KWA KUMNG'ATA BINADAMU NA KUFARIKI DUNIA NA KUJERUHI TABORA.

Tabora. Kikosi cha Kuzuia Ujangili Kanda ya Magharibi kinamsaka fisi mmoja kati ya wawili waliowashambulia Samwel Gamalaya na kusababisha kifo chake na kumjeruhi Kusekwa Ngeleja wakati wakikata kuni katika pori lililopo Kitongoji cha Isukamahela Manispaa ya Tabora.

Fisi hao wawili walimshambulia kwa kumng’ata Gamalaya maeneo mbalimbali ya mwili na kusababisha kifo chake, huku wakimjeruhi Ngeleja mikono na miguu.

Kamanda wa Kikosi cha Kuzuia Ujangili Kanda ya Magharibi, Charles Msilanga alisema jana (juzi) kuwa baada ya polisi kumpiga risasi fisi mmoja na kumuua, mwingine alikimbia.



Alisema wanaendelea kumsaka fisi huyo ili kuzuia madhara zaidi kwa wakazi wa kitongoji hicho.

“Fisi aliyekimbia anaweza kuleta madhara kwa watu na ndiyo maana tunamsaka kwa udi na uvumba,” alisema Msilanga.

Mwenyekiti wa kitongoji hicho, Iddi Cheyo alisema Gamalaya alifariki dunia baada ya kukaa muda mrefu bila matibabu tangu aliposhambuliwa na fisi hao.

Baadhi ya wakazi wa kitongoji hicho, Sophia William na Juma Kapambala walisema tukio hilo limewastaajabisha kwani kwa miaka mingi wanafanya shughuli zao ndani ya msitu huo bila kushambuliwa na wanyama.

“Tunafanya shughuli zetu katika msitu huu kwa miaka mingi bila kuvamiwa, lakini hatujaona mnyama kuingia eneo hilo,” alisema Sophia.
kwa hisani ya MWANANCHI








MUHIMU KWAKO....!!!
kama wewe ni mtafutaji wa kujitegemea au unatarajia kuja kuwa.... zingatia hii

JOINT SCOPE LTD imedhamiria kutoa msaada wa ushauri bure, kwa wanaotarajia au wanataka kusajili BUSINESS NAME au COMPANY LIMITED n.k.
 
hapa utaelezwa mchakato mzima na kila kinachohitajika wakati utakapotaka kufanya usajili wa kampuni au Jina la Biashara kupitia Brela, ambayo ndiyo mamlaka pekee Tanzania yenye mdhamana ya kusajili Kampuni (Company LTD) na Jina la Biashara (Business Name), Logo n.k.
 
Tumeamua kutoa huduma hii ya ushauri bure kutokana na kero za matapeli tulizokutana nazo na tulishindwa kuwatambua kutokana  na kutoweza watambua kwa kutojua ukweli halisi wa vinavyohitajika wakati wa usajili wa Kampuni ya JOINT SCOPE LTD.
 
"Ni vyema Kutafuta Elimu ya Jambo Unalotaka Kufanya Kwanza Kabla ya Kuanza Kufanya"

Kwa Mawasiliano
Simu: 0712 479 905

E-mail; jointscope@gmail.com

P.O. Box 2574 Morogoro - Tanzania

Huduma hii ni Bure kwa watanzania Tu!

ToGether We Can.....!!!!!
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

0 comments:

Item Reviewed: FISI WASAKWA NA KIKOSI CHA KUZUIA UJANGILI KWA KUMNG'ATA BINADAMU NA KUFARIKI DUNIA NA KUJERUHI TABORA. Description: Rating: 5 Reviewed By: mcjohnminja.blogspot.com
Scroll to Top