WAZIRI
MKUU Kassim Majaliwa amepokea misaada mbalimbali kwa ajili ya wakazi wa
vijiji vya Mtondo na Nanjaru wilayani Ruangwa mkoani Lindi ambao nyumba
zao ziliezuliwa na upepo Januari mwaka huu.
Akizungumza
na wananchi wa vijiji hivyo (Jumapili, Februari 28, 2016), Waziri Mkuu
alisema maafa huwa yanakuja bila kutarajiwa na akatumia fursa hiyo
kuwashukuru wadau waliotoa misaada ya chakula, magodoro, mashuka,
vitenge, mabati na mbegu za mazao.
Aliwataja
wadau hao kuwa ni benki ya NMB, NSSF, wakazi wa Ruangwa na marafiki wa
Ruangwa waishio Dar es Salaam ambao walifika kukabidhi misaada hiyo.
Waziri
Mkuu ambaye yuko kwenye ziara ya siku mbili katika mikoa ya Mtwara na
Lindi kukagua athari za mafuriko, hatua zinzochukuliwa za utoaji
misaada kwa waathirika na kuwapa pole wananchi walioathirika na mafuriko
hayo, alitumia fursa hiyo kuwataka wananchi waishio mabondeni wahame
kwa sababu mvua kubwa bado zinakuja.
“Jambo
hili si mipango ya mtu binafsi na sote tunajua kwamba tunahitaji mvua
kwa ajili ya mazao lakini safari hii zimekuja zaidi ya kiwango cha
kawaida. Mamlaka ya hali ya hewa imeshasema kuwa mvua kubwa zaidi
zinakuja ifikapo Machi mwaka huu”, alisema.
Ili
kuepusha maafa zaidi, kuanzia sasa, wale waliojenga mabondeni wanapaswa
wahame. Pia nawasihi wananchi wachukue tahadhari wakiona mvua inakuja
na upepo mkali wasikae ndani ya nyumba sababu hapa kijijini tumempoteza
mzee wetu mmoja ambaye aliangukiwa na nyumba baada ya nyumba yake
kuangukiwa na mti kutokana na mvua hizo,” aliongeza.
Kwa
mujibu taarifa ya maafa iliyotolewa na Mkuu wa wilaya ya Ruangwa, Bi.
Mariam Mtima, mvua zilizonyesha kati ya Januari na Februari mwaka huu
zilisababisha nyumba 393 kuezuliwa na nyingine kubomoka na kuacha wakazi
wa vijiji hivyo bila makazi.
“Zahanati
ya kijiji cha Mtondo iliezuliwa paa, daraja la mto Muhuru limebomoka na
halipitiki kabisa na ekari 1,186 za mashamba ya wananchi zimesombwa na
maji. Mazao yaliyoathirika ni mahindi, muhogo, mikorosho, mtama, ufuta,
kunde, mpunga na mbaazi,” alisema Mkuu huyo wa wilaya katika taarifa
yake.
Alivitaja
vijiji vingine ambavyo mafuriko hayo yaliharibu mashamba ya wananchi
kuwa ni Nambilanje, Mkaranga, Namkatila, Chinongwe A, Likwachu, Nauname
na Mbekenyera.
Alisema
hali hiyo imesababisha upungufu mkubwa wa chakula wilayani humo na sasa
hivi wanahitaji tani 1,133 za chakula aina wanga ambazo anataraji
zitatosheleza mahitaji kwa mwezi Machi 2016.
IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU.
Waziri
Mkuu, Kassim Majaliwa akizindua ujenzi wa zahanati ya kijiji cha
Nandagala wilayani Ruangwa ambao unafanywa kwa ufadhili wa kampuni ya
HUAWEI ya China , kijijini hapo, Februari 28, 2016. Kulia kwake ni Mkuu
wa Mkoa wa Lindi, Jordan Lugimbana.
MUHIMU KWAKO....!!!
kama wewe ni mtafutaji wa kujitegemea au unatarajia kuja kuwa.... zingatia hii
JOINT SCOPE LTD imedhamiria kutoa msaada wa ushauri bure, kwa
wanaotarajia au wanataka kusajili BUSINESS NAME au COMPANY LIMITED n.k.
hapa utaelezwa mchakato mzima na kila kinachohitajika wakati utakapotaka
kufanya usajili wa kampuni au Jina la Biashara kupitia Brela, ambayo
ndiyo mamlaka pekee Tanzania yenye mdhamana ya kusajili Kampuni (Company
LTD) na Jina la Biashara (Business Name), Logo n.k.
Tumeamua kutoa huduma hii ya ushauri bure kutokana na kero za matapeli
tulizokutana nazo na tulishindwa kuwatambua kutokana na kutoweza
watambua kwa kutojua ukweli halisi wa vinavyohitajika wakati wa usajili
wa Kampuni ya JOINT SCOPE LTD.
"Ni vyema Kutafuta Elimu ya Jambo Unalotaka Kufanya Kwanza Kabla ya Kuanza Kufanya"
Kwa Mawasiliano
Simu: 0712 479 905
E-mail; jointscope@gmail.com
P.O. Box 2574 Morogoro - Tanzania
Huduma hii ni Bure kwa watanzania Tu!
ToGether We Can.....!!!!!
0 comments:
Post a Comment