![]() |
Nguchiro-Jangwa |
Na Lwitiko Peter
NGUCHIRO ni mnyama mdogo jamii ya panya, anayepatikana kwa wingi barani Afrika na kusini mwa mabara ya Ulaya na Asia.
Kuna kama jamii 33 hivi za nguchiro. Lakini kuna jamii nyingine nne za ziada ambazo hupatikana huko Madagascar.
Hawa
ni jamii ndogo ya Galidiinae. Awali, jamii hizi nne ziliwekwa katika
kundi la wanyama wengine wanaopatikana huko Madagascar lakini baadaye
ikaja kujulikana kuwa wana sifa tofauti, hivyo kuundiwa makundi yao
yanayojitegemea.
Utafiti
wa kijenetiki unaonyesha kuwa Galidiinae wana uhusiano wa karibu na
wanyama wengine wa familia ya Eupleridae, ambao wanakaribiana sana na
nguchiro.
Mwonekano
Kama
tulivyodokeza hapo juu, nguchiro hupatikana kwa wingi katika maeneo ya
Afrika na kusini mwa Ulaya na Asia. Lakini pia kwa kiasi kidogo
hupatikana huko Puerto Rico na sehemu ya visiwa vya Caribbean na
Hawaiian.
Lakini huko walipelekwa kama wanyama wa kufugwa na kupambana na wanyama waharibifu na hatari kama vile panya na nyoka.
Kuna
jamii kuu 33 za nguchiro ambao kwa wastani ukubwa wao ni kati ya futi
moja na nne kwa urefu. Uzito wa nguchiro unatofautiana sana kulingana na
jamii husika.
Wapo nguchiro wadogo ambao uzito wao ni kama gramu 280 tu wakati wapo wengine wakubwa ambao hufikia uzito wa zaidi ya kilo nne.
Baadhi ya jamii ya nguchiro huishi maisha ya upweke huku kila mmoja akijitafutia chakula chake mwenyewe.
Lakini
zipo jamii nyingine ambazo nguchiro huishi katika kundi kubwa,
wakisafiri na kufanya mambo mengine pamoja kama vile kutafuta na
kugawana chakula.
Nguchiro anafanana sana na mnyama mwingine ajulikanaye kama
Mustelids.
Wote wana sura ndefu na miili mirefu pia. Wana masikio madogo ya duara,
miguu mifupi na mikia mirefu. Wengi wana manyoya machache sana mwilini,
ni wachache tu ndio wana manyoya mengi.
Vidole
vyake vina kucha lakini kucha hizi hutumika sana kwa ajili ya kazi ya
kuchimba. Kama ilivyo kwa mbuzi, nguchiro wana macho madogo sana.
Wengi
wa jamii za nguchiro wana vifuko kwenye sehemu yao ya makalio vyenye
kemikali inayotoa harufu ambayo huitumia kuweka mipaka na himaya ya
maeneo yao. Pia, harufu hii hutumika kuashiria kuwa mnyama fulani yupo
tayari kwa ajili ya kujamiiana.
Kama
ilivyo kwa nyoka, nguchiro naye ana aina fulani ya mfumo ambao unazuia
mwili wake kudhurika na sumu. Wataalamu bado wanaendelea kutafi iwapo
hii ndiyo sababu mnyama huyu hadhuriki na sumu ya nyoka.
Historia
![]() |
Nguchiro mwembamba (Galerella sanguinea)
|
Tofauti
na wanyama wanaofanana naye kama vile viverrids, nguchiro ni mnyama
ambaye hufanya shughuli zake nyakati za mchana wakati wale wengine
hujishughulisha zaidi usiku.
Nguchiro
wa Misri ndiye anayetambulika kama nguchiro anayependa kutembea peke
yake. Hata hivyo, kuna wakati nguchiro hawa nao hutembea katika makundi.
Nguchiro
jamii ya Meerkat au kwa jina jingine Suricate (Suricata suricatta),
ambao wana umbo dogo, wanaishi katika makundi ya hadi wanyama kati ya 20
na 30.
Katika
kila kundi kunakuwa na dume mkubwa mmoja na jike wake. Huwa
wanaambatana na watoto wao na vijukuu na vitukuu. Hawa hupatikana pia
katika maeneo ya wazi huko kusini mwa Afrika katika nchi kama Angola,
Namibia, Botswana na Afrika Kusini.
Jamii
nyingine ya nguchiro ijulikanayo kama meerkat; ni wadogo kwa umbo ambao
chakula chao kikuu ni wadudu na wanyama wadogo wadogo na nyoka. Udogo
wa umbo na uzito mdogo ni mambo yanayomfanya awe hatarini sana
kushambuliwa na wanyama wakubwa walao nyama na hata ndege wakubwa kama
tai. Hata hivyo, naye huwakamata ndege wadogo wadogo na kuwala.
Kama njia ya kujilinda katika kundi, nguchiro mmoja hufanywa mlinzi wakati wengine wakitafuta chakula.
Huyu hukaa sehemu iliyoinuka na kusimama kwa miguu miwili ya nyuma ili kumwezesha kuona mbali na pande zote.
Anapoiona
hatari, hutoa sauti kali ili kuwashitua wenzake kuwa kuna hatari
inawanyemelea. Pamoja na sauti hiyo pia hutoa ishara hatari inatokea
upande gani, kama ni angani au ardhini ili kuwawezesha wenzake kuchukua
hatua zinazofaa kujilinda.
Chakula
Chakula kikuu cha nguchiro ni wadudu, kaa, minyoo, mijusi, nyoka, ndege na panya. Pia hula mayai.
Nguchiro
wa kijivu wa huko India na wengine wanafahamika kwa uwezo wao mkubwa wa
kuwashambulia na kuwaua nyoka hata wale wenye sumu kali kama vile
cobra.
Inaaminika kuwa wanaweza kufanya hivi kutokana na ukali wao na ngozi yao ngumu.
Lakini
kikubwa zaidi ni kemikali iliyomo mwilini mwao, ambayo inazuia sumu ya
nyoka kuingia kwenye damu na misuli. Ingawa nguchiro ana uwezo wa
kuwinda nyoka, lakini mara nyingi hujiepusha sana kuwinda cobra.
![]() |
Nguchiro miriba |
Nguchiro pia anaweza kufugwa na kutumika kama mnyama wa kupambana na panya ndani ya nyumba kama vile anavyotumika paka.
Hata
hivyo, pamoja na kuzuia panya, nguchiro anayefugwa anaweza kuwa
mwaribifu. Wakati nguchiro walipopelekwa huko West Indies kwa ajili ya
kuua nyoka na panya, waliharibu pia mimea hasa ile midogo midogo ambayo
nayo huitafuna kama sehemu ya mlo wao.
Kutokana
na sababu hii, hivi sasa ni kinyume cha sheria kupeleka aina yoyote ya
nguchiro huko Marekani na Australia. Nguchiro walipelekwa katika Kisiwa
cha Hawaii mnamo mwaka 1883 na tangu wakati huo wameonekana kuwa na
madhara kwa wanyama wenyeji wa eneo hilo.
Uhusiano na binadamu
Nguchiro
hupenda sana kuishi karibu na makazi ya watu. Hivyo mara nyingi
huonekana wakikatiza barabara na nyakati za usiku wengi hugongwa na
magari.
Huko
Pakistan, watu wanaocheza na nyoka huwafuga nguchiro na kuwafundisha
kupigana na nyoka na huwatumia kama sehemu ya michezo yao.
Zamani
huko Okinawa nchini Japan, nguchiro waliletwa ili kupambana na nyoka
aitwaye Habu, lakini kutokana na mbinyo wa watetezi wa haki za wanyama,
suala hilo limeachwa siku hizi.
0 comments:
Post a Comment