Baada
ya mchezo wa fainali ya kombe la Carling na Manchester City kuibuka na
ushindi dhidi ya Liverpool katika hatua ya penati timu hizo zimekutana
tena usiku wa kuamkia Alhamisi katika mchezo wa Ligi Kuu ya Uingereza.
Mchezo huo
ulimalizika kwa Liverpool kuibuka na ushindi wa goli tatu kwa bila,
magoli ya Liverpool yakifungwa na Adam Lallana dakika ya 34, James
Milner dakika ya 45 na Roberto Firmino katika dakika ya 57.
Baada
ya ushindi huo, Liverpool imefikisha alama 41 na kushika nafasi ya 8 ya
msimamo wa ligi ya Uingereza huku Manchester City ikisalia katka nafasi
ya nne ikiwa na alama 47.
Matokeo ya michezo mingine iliyopigwa jana usiku ni;
Arsenal 1 – 2 Swansea City
Stoke City 1 – 0 Newcastle United
West Ham 1 – 0 Tottenham
Manchester United 1 – 0 Watford
0 comments:
Post a Comment