Mapacha wa kipekee wamezaliwa nchini Vietnam.
najua unajiuliza mapacha si kawaida tu ? La hasha .
Mapacha hawa imegunduliwa kuwa walitungwa na baba wawili tofauti !
Amini usiamini !
Taarifa zinasema familia za mapacha hao iligundua kuwa watoto hawakufanana hata kidogo.
Kwa hivyo ikawalazimu kufanyiwa uchunguzi wa celi za DNA.
Mbivu na mbichi ilipobainika, Watoto hao walipatikana kuwa hawana uhusiano wa aina yeyote!
Taasisi ya utafiti wa maumbile{ Genetic Association} inasema hali kama hii hufanyika japo siyo kawaida.
Mwanamke anaweza kupata mapacha na baba wawili tofauti ikiwa atajamiana na wanaume wawili katika kipindi cha siku chache wakati ambapo mayai yake yameiva.
Kulingana na profesa Dinh Luong ,mtafiti mkuu wa taasisi ya utafiti wa seli na jeni nchini Vietnam matokeo ya uchunguzi wa jeni ulibaini asilimia 100% kuwa watoto hao hawakuwa wa baba mmoja.''Inawezekana kuwa binti huyo alikuwa katika siku ambayo mayai yake yalikuwa yameiva kwa kawaida mwanamke akiwa hapo anashikwa na uchu kwa sababu mwili wake unatoa mayai na unataka mwanamume atakaye mpa shahawa''
''kwa sasa tunaamini kuwa bibi huyo alilala na wanaume wawili tofauti katika siku hiyo hiyo ambapo mayai yake yalikuwa tayari na hivyo akatungwa mimba na wanaume wawili.''
''Hili linaweza kutokea ila ni tukio nadra sana'' alisema Profesa Luong.
Matukio kama hayo ni machache mno.
''Kitaaluma kuna takriban wanawake 10 pekee duniani ambao wamewahi kutungwa mimba na wanaume wawili kwa wakati mmoja.''
Kuna visa 10 pekee vya mapacha waliozaliwa na baba tofauti duniani, huenda kuna hali kama hiyo lakini pengine wazazi huwa hawaelewi, imeongeza taasisi hiyo.
Vyombo vya habari vya Vietnam vilianza kuripoti kuhusu mapacha hao baada ya mmoja wa jamaa wao kusema pacha mmoja hakufanana kabisa na mwenzake pia na wakiwemo wazazi.
Profesa huyo hakutaka kuendelea kuelezea kwa sababu aliohofia angekiuka haki za mgonjwa wake na hata kuvunja ndoa.
Mapacha hao wa kipekee waligonga vichwa vya habari kutokana na utofauti wao mkubwa na wazazi wao.BBC
0 comments:
Post a Comment