Waziri
wa Uingereza anayeshughulikia masuala ya Afrika, Mhe. James Duddrige
akimueleza jambo Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Ajira
na Watu wenye Ulemavu), Mhe. Jenista Mhagama (Mb), tarehe 08 Machi,
2016, Jijini Dar es Salaam.
Waziri
wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Ajira na Watu wenye
Ulemavu), Mhe. Jenista Mhagama (Mb), akimueleza jambo Waziri wa
Uingereza anayeshughulikia masuala ya Afrika, Mhe. James Duddrige
(hsyupo pichani), tarehe 08 Machi, 2016, Jijini Dar es Salaam.(Picha zote na Ofisi ya Waziri Mkuu).
Waziri
wa Uingereza anayeshughulikia masuala ya Afrika, Mhe. James Duddrige
(wa kwanza kulia) akimsikiliza Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu
(Sera, Bunge, Ajira na Watu wenye Ulemavu), Mhe. Jenista Mhagama (Mb),
(hayupo pichani) alipokutana naye Ofisini kwake, tarehe 08 Machi, 2016,
Jijini Dar es Salaam.
Hayo yamesemwa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Ajira na Watu wenye Ulemavu), Jenista Mhagama ambaye alimwakilisha Waziri Mkuu, Majaliwa Kassim Majaliwa kufanya mazungumzo na Waziri wa Uingereza anayeshughulikia masuala ya Afrika, Mhe. James Duddrige, leo jioni, terehe 08 Machi, 2016, Jijini Dar es salaam.
“Tunatarajia mpango huu ukishafanyiwa maboresho utaimarisha uchumi wa nchi zote mbili, tunatarajia baada ya maboresho hayo makampuni mengi kutoka uingereza kuja kufanya biashara nchini kuwekeza .Tunaelewa nia ya serikali ya Uingereza kuwekeza katika miundo mbinu iliyopo vijijini hasa katika sekta ya maji na kilimo hii itasaidia kuinua maisha ya wananchi wanaoishi vijijini hasa wanawake , hii ni kutokana na kuwa asilimia 80 ya wananchi nchini wanaishi vijijini na wengi wao ni wananawake na leo ukizingatia ni siku ya wanawake Duniani” Alisema Mhagama.
Aliongeza kuwa mpango huo umekuja muda muafaka wakati serikali inaendelea na juhudi za kuishirikisha sekta binafsi katika kukuza uchumi nchini kwa kuwa serikali inatambua sekta binafsi ndio chachu ya maendeleo nchini.
“Tunahitaji ushirikiano wenu ili muweze kutujengea uwezo wa kuwavutia wawekezaji wa ndani na wa kimataifa kwa msingi wa kuendeleza viwanda nchini na hatimaye tunaweza kufanya kwa ubora biashara kimataifa ” alisistiza.
Tanzania
na Uingereza zinatarajia kuendelelea kushirikiana katika masuala ya
Uchumi kupitia Mpango wa Ushirikiano wa Kiuchumi kati ya Tanzania na
Uingereza “UK partnership in Prosperity” ambao unajikita katika maeneo
makubwa ya ushirikiano ya Mafuta na Gesi, Nishati Jadidifu; Kilimo; na
Uboreshaji Mazingira ya Biashara.
Hayo yamesemwa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Ajira na Watu wenye Ulemavu), Jenista Mhagama ambaye alimwakilisha Waziri Mkuu, Majaliwa Kassim Majaliwa kufanya mazungumzo na Waziri wa Uingereza anayeshughulikia masuala ya Afrika, Mhe. James Duddrige, leo jioni, terehe 08 Machi, 2016, Jijini Dar es salaam.
“Tunatarajia mpango huu ukishafanyiwa maboresho utaimarisha uchumi wa nchi zote mbili, tunatarajia baada ya maboresho hayo makampuni mengi kutoka uingereza kuja kufanya biashara nchini kuwekeza .Tunaelewa nia ya serikali ya Uingereza kuwekeza katika miundo mbinu iliyopo vijijini hasa katika sekta ya maji na kilimo hii itasaidia kuinua maisha ya wananchi wanaoishi vijijini hasa wanawake , hii ni kutokana na kuwa asilimia 80 ya wananchi nchini wanaishi vijijini na wengi wao ni wananawake na leo ukizingatia ni siku ya wanawake Duniani” Alisema Mhagama.
Aliongeza kuwa mpango huo umekuja muda muafaka wakati serikali inaendelea na juhudi za kuishirikisha sekta binafsi katika kukuza uchumi nchini kwa kuwa serikali inatambua sekta binafsi ndio chachu ya maendeleo nchini.
“Tunahitaji ushirikiano wenu ili muweze kutujengea uwezo wa kuwavutia wawekezaji wa ndani na wa kimataifa kwa msingi wa kuendeleza viwanda nchini na hatimaye tunaweza kufanya kwa ubora biashara kimataifa ” alisistiza.
0 comments:
Post a Comment