Kikosi
cha timu ya Taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’ kinachodhaminiwa na bia ya
Kilimanjaro Premium Lager, kinatarajiwa kuwasili leo saa 8 usiku katika
uwanja wa ndege wa kimataifa wa Mwl. JK Nyerere kikitokea nchini Chad
kilipokuwa na mchezo dhidi ya wenyeji jana jioni.
Msafara
wa Taifa Stars unaongozwa na mkuu wa msafara ambaye pia ni Rais wa Chama
cha Soka Zanzibar (ZFA), Ravia Idarus Faina utaondoka uwanja wa ndege
wa kimataifa wa N’Djamena saa 8 mchana kuelekea Addis Ababa nchini
Ethiopia, kabla ya kuunganisha ndege saa 4 usiku tayari kwa safari ya
kurejea nyumbani Tanzania.
Stars
inarejea nyumbani baada ya kuibuka na ushindi wa bao 1–0 dhidi ya
wenyeji Chad, bao lililofungwa na nahodha Mbwana Samatta katika mchezo
uliochezwa uwanja wa Omnisport Idriss Mahaymat Ouya jijini N’Djamena
katika mchezo wa kundi G kuwania kufuzu kwa Fainali za Mataifa Afrika
(AFCON) mwaka 2017.
Mara
baada ya kuwasili jijini Dar es salaam, kikosi cha Taifa Stars kitaingia
moja kwa kwa moja kambini katika hoteli ya Urban Rose iliyopo eneo la
Kisutu kujiandaa na mchezo wa marudano utakaochezwa siku ya Jumatatu ya
Pasaka katika uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam.
0 comments:
Post a Comment