HATUNA budi
kumshukuru Mwenyezi Mungu kwa kutukutanisha tena katika uwanja wetu
maridhawa wa kupeana darasa la uhusiano. Siku zote ukikubali kupokea na
kufanyia kazi yale tunayopeana kila Jumamosi kupitia safu hii.
Mada yetu iliyohusu mke wa mtu kuwa
mke wa watu. Nilieleza namna ambavyo mke wa mtu anavyoweza kuangukia
katika dmbwi la kuwa mke wa watu kwa sababu ya kukosa umakini.
Anashindwa kujua kwamba kama mke wa
mtu anapaswa aishi vipi na ndugu, jamaa na marafiki ili asitoe mwanya wa
watu kumfanya mke wa watu.Tumalizie mada hii kwa kutazama mazingira na
vichocheo vinavyowasababisha mke wa mtu ageuke kuwa mke wa watu. Mbali
na kujua vichocheo hivyo, pia tutapata kujua mbinu mbalimbali za
kuepukana na tatizo hili:
UMBALI
Unapokuwa umeolewa moja kwa moja
utakutana na mashemeji utakutana na marafiki wa kiume kama vile
ulivyokuwa hujaolewa. Suala la msingi hapa ni mabadiliko. Unatakiwa
kubadilika ili usiweze kutoa mwanya wa vishawishi.
Kama mtu ni shemeji yako, muwekee
mipaka yake. Usikae naye kama vile unavyokaa na mumeo. Hata kama yeye
ataleta ukaribu, wewe ndiyo unatakiwa kuweka mipaka. Ukiruhusu
akukaribie, utarusu akushike na baadaye anaweza kufikia hatua ya kula
tunda analokula kaka yake.
Epuka mazoea yasiyo kuwa na tija.
Mazoea ndiyo yale ndiyo yanaletaka ‘shemeji shemeji huku mwazima
taa.’Utani unaanzaga taratibutaratibu, unaota mizizi na baadaye mnafanya
kweli. Mtu ambaye si mume wako, hakikisha hakukaribii. Mpe salamu,
zungumza naye lakini asiwe karibu kupindukia.
KIPAUMBELE
Kama binadamu, wanawake nao wana matamanio. Anaweza kuvutiwa na kitu fulani kutoka kwa mtu fulani ambacho pengine mumewe hana. Ataanza kwa kuvutiwa, baadaye atataka kuonana naye na mwishoni wanajikuta ni wapenzi.
Kama binadamu, wanawake nao wana matamanio. Anaweza kuvutiwa na kitu fulani kutoka kwa mtu fulani ambacho pengine mumewe hana. Ataanza kwa kuvutiwa, baadaye atataka kuonana naye na mwishoni wanajikuta ni wapenzi.
Mke anayejiheshimu hawezi kumpa
kipaumbele mwanaume mwingine yeyote kwa kigezo chochote. Mumewe ndiyo wa
kwanza katika hali yoyote. Hata kama mwanaume fulani ana fedha kuliko
mumewe, ana sifa ya ziada kuliko mumewe, anapaswa kusema mumewe ndiyo
zaidi.

KUTOTOA SIRI
Mwanamke ambaye hana heshima hutoa
siri za ndani. Kama mumewe ana tatizo fulani, analiweka wazi kwa
marafiki wa kiume wa mumewe pasipo kujua anatoa mwanya wa kutongozwa.
Wanaume wajanja wanasoma udhaifu, wanakutimizia na furaha yako
inaendelea kuwepo bila ya mumeo.
Tunza siri. Kama kuna tatizo la
faragha, jaribu kuzungumza na mwenzako ili mtafakari kwa pamoja kuhusu
suluhu. Kama ni tatizo linaloweza kutibika hospitali, nendeni mkapate
ushauri wa kitabibu.
Ni matumaini yangu endapo
utayazingatia hayo tuliyoyadili, hakikaka huwezi kuwa mume wa watu bali
utakuwa mume wa mtu mmoja ambaye mtaishi kwa upendo, amani na furaha.
0 comments:
Post a Comment