Miriam Lukindo ni Mwanamuziki wa nyimbo za injili kutoka nchini Tanzania,
Miriam ambaye tofauti na uimbaji hufanya kazi za upambaji maofisini na
katika matukio mbali mbali, alikulia katika jiji la mbeya ambako alikuwa
akiishi yeye mama yake pamoja na bibi yake.
Miriam alisoma shule ya msingi Kilimo Uyole na kufanikiwa kuendelea na masomo ya sekondari katika shule ya sekondari majengo iliyoko katikati ya mji wa Moshi.
Miriam alisoma shule ya msingi Kilimo Uyole na kufanikiwa kuendelea na masomo ya sekondari katika shule ya sekondari majengo iliyoko katikati ya mji wa Moshi.
Mama
yake na Miriam alipata ujauzito ulipelekea kuzaliwa kwa Miriamu akiwa
kidato cha Pili(form II), kwa wakati huo alikuwa na umri wa miaka kumi
na sita (16) tu. Katika kipindi chote hicho toka akiwa mdogo Miriam
aliiambia Hosanna Inc kuwa alikuwa akipenda sana kuimba na alikuwa akipenda sana kusikiliza na kuimba nyimbo za Rebeka Malope.
Kwa kipindi chote hicho Miriam hakuwahi kumfahamu baba yake japokuwa aliambiwa kuwa yupo. Jambo hilo
lilimuumiza na ilifikia hatua akaona ni hali ya kawaida hivyo chochote
kuhusu yeye bibi yake na mama yake ndio walikuwa kila kitu kwake.
Mwaka
1995 mwezi wa kumi na mbili(December), kwa mara ya kwanza Miriamu
alipata fursa ya kunana uso kwa uso na baba yake mzazi Mzee Lukindo.
Miriam anasema pamoja na maongezi yote anakumbuka alimwambia babaye neno
moja la msingi kuwa “ Nimefurahi kukujua ”
Miriam akitoa msaada kwenye kituo cha watoto wadogo wenye mtindio wa ubongo jijini Dar es salaam |
Baada ya masomo yake ya sekondari Miriamu alipata nafasi ya kundelea na masomo ya chuo katika jiji la Nairobi nchini Kenya. Kwa mujibu wa Miriam akiwa nchini humo ndipo hasa kipaji chake cha uimbaji kiliweza kuchanua vizuri .Akiwa nchini Kenya
alikuwa akisali katika kanisa la Maximum Miracle Centre lililo chini ya
Mchungaji na muimbaji mahiri nchini humo aitwaye Pastor Pius Muiru.
Chini
ya Pastor Muiru Miriam alikuwa kingozi wa sifa na kuabudu kanisani
hapo. kanisa hil ndilo mzizi wa kundi Maarufu la muziki wa injili nchini
humo liitwalo Maximum Melody. Katika kipindi hicho Miriam anasema
alipitia masaibu mengi ya kumkatisha tamaa kimaisha lakini Kristo
alikuwa akimtetea na hatimaye alifanikiwa kurekdi album yake ya Kwanza aliyoiita Amen Amen mwaka 2000
Baada ya kurekodi album hiyo nchini Kenya, Miriam aliamua kurudi nyumbani Tanzania. Alipofika Tanzania
kwa kuwa Baba yake na Mama yake hawakuwa pamoja na bibi yake akiwa
mbeya ilimuwia vigumu namna ya kuweza kuishi katika jiji la Dar es
salaam. Kwa bahati rafiki yake mmoja alikubali kuishi naye. katika
kipindi hicho Miriam aliamua kufanya huduma kwa nguvu na Album yake
ilkubaliwa vyema na watu mbali mbali hivyo kwa sehemu ikawa Faraja kwa
Miriam.
mahojianono na Miriam Lukindo katika Hotel ya Sparrow |
Miriam
anasema moja kati ya changamoto alizokutana nazo katika huduma yake ni
kutunga nyimboo na kujikuta watu wengine wakiingia studio na kuzirekdi.
Anasema miaka ya nyuma alitunga nyimbo maarufu iitwayo ya NIGUSE TENA,
pamoja na SEMA NA MOYO WANGU na kwa kuwa zilikuwa zake hivyo aliziimba
Live mara kwa mara alipokuwa akiitwa kufanya huduma, na kipindi hicho
ndipo kundi maarufu la Krystaal lilikuwa nchini Tanzania.
Miriam akiwa na mwanamuziki wa injili Marion Shanko toka nchini kenya |
Mwaka
2005 krystaal walipokuja Tanzania kwenye mkutano wa Mwakasege ambapo
Miriam nayeye alialikwa kuhudumia, Miriam aliwauliza kwa nini mliamua
kurekodi nyimbo hizo pasipo kuniambia, Krystaal wa walimjibu kuwa
walijua kuwa hizo ni pambio tu hivyo wakaamua kuzichukua na kuzirekodi
serius.
Mwaka
2005 Miriam alifunga ndoa na mhadhili wa chuo kikuu cha Dar es salaam
(UD) na Mwanasaikolojia maarufu nchini aitwaye Chriss Mauki. Chriss kwa
sasa yuko nchini Afrika ya kusini akisomea shahada ya Uzamivu(Ph.D).
Miriam anasema mara baada ya kuolewa aliamua kutulia kidogo pasipo kutoa
album ili aweze kujifunza maisha ya ndoa, miaka miwili baadaye yaani
Mwaka 2008 akishirikiana na mumewe aliweza kutoa album aliyoipa jina la
Ni Ahsubuhi.
Miriam Lukindo akiwa na Mumewe Chriss Mauki |
Aliamua
kuipa album hiyo jina hilo kwa kuwa aliona kuwa anaanza upya kwa kila
kitu katika maisha yake. Hii ni baada ya kupitia mapito mbalimbali hivyo
aliona ni kama maisha yameanza upya hivyo ni asubuhi.
Album
hiyo hakuifanyia video mpaka mwaka jana 2010 ambapo alianza kushoot
video ya album yake hiyo chini ya kampuni ya Haak Neel Prductin. Miriam
kwa sasa yuko chni ya Lebo ya kampuni hiyo, na alifanikiwa kuzindua
video ya album hiyo mwaka huu mwezi wa nne katika ukumbi wa Diamnd
Jubelee.
Miriam Lukindo akiwa jukwaani wakati wa uzinduzi wa album yake ya Ni Asubuhi katika uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza |
Yafuatayo ni maswali na majibu baina ya Hosanna Inc pamoja na Miriam
Swali: Katika
labum yako ya Ni Asubuhi kwa nini ulimchagua Jackson Benty kuimba
pamoja nawe ilihali Tanzania kuna waimbaji wengi wa kiume?
Miriam: Ni kweli Tanzania kuna waimbaji wengi wazuri lakini nilimchagua Benty kwa kuwa Benty analadha ya Worship, Benty ni worshiper.
Swali:Kwa
mtu anayekufahamu au kukufuatilia katika huduma yako ya uimbaji,
anaweza kukubaliana na Hosanna Inc kuwa Miriam umekuwa ukifanya vizuri
sana katika nyimbo za kuabudu(worship) kuliko nyimbo za sifa(Praise),
nini hasa kinachopelekea hali hiyo?
Miriam: Mimi nafanya muziki wowote sifa, pamoja na kuabudu, ila
ni kweli kwenye eneo hilo nimekuwa nikifanya vizuri zaidi kwa kuwa
katika huduma yangu Mungu alinitamkia kuwa ”kwenye Worship ndio nitakaa
hapo”
Swali: Kitu gani kilichopelekea utunge wimbo wa Anasikia?
Miriam:
Kuna kipindi nilikuwa nasafiri wakati niko Kenya na sikuwa na pesa ya
kutosha hivyo niliomba msaada kwenye yale magari makubwa ya mizigo, wao
waliniambia kama unaweza kaa huko nyuma pamoja na mizigo, nami
nikakubali hivyo nikiwa humo ndani ya Lorry ndipo idea ya wimbo huo
ikaja kuwa Mungu anasikia.
Swali; Tumeshuhudia waimbaji wengi wanakuja na kupotea lakini wewe toka miaka hiyo ya 2000 mpaka leo upo katika huduma hii, nini hasa kinachokufanya ubakie katika ene hili la uimbaji?
Miriam:
Kwa kifupi ni lazima ujue wewe ni nani kwa mantiki ya kujua misingi ya
huduma uliyonayo Je umeitwa au umechaguliwa kuifanya huduma hiyo? Mi
nina wito na huduma hii ndio maana mpaka leo natumika katika eneo hili.
swali: Kwa nini uliamua kufanya video na Haak Neel Prductin na si kampuni lingine?
Miriam:
Kuna makampuni mengi yalinifata ili kufanya nayo video lakini sikuwa
radhi kufanya hivyo kwa kuwa kuna kiwango fulani cha ubora nilikuwa
nakitaka. Walipotokea Haak Neel niliona ndio wenye uwezo huo kwa kuwa
wanavifaa vya kutosha, pia hawana utaratibu wa muda kuwa tunafanya video
kwa wiki moja tu na kumaliza, lakini hawa tunafanya na na kurudia kadri
tuwezavyo. Hii album ya Ni Asubuhi ina nyimbo nane, na nimeshoot nao
kwa miezi tisa sasa unaweza jionea tofauti.
Tunamtakia kila la heri Miriam na Familia yake katika huduma ambayo Mungu amewaitia.
0 comments:
Post a Comment