Msanii
wa muziki wa dansi Ndanda Kosovo amefariki dunia asubuhi ya leo katika
hosptali ya taifa ya Muhimbili alipokuwa akipatiwa matibabu.
Kwa
mujibu wa taarifa kutoka kwa mwanamuziki mwenzake Kardinal Gento,
Ndanda alikuwa alisumbuliwa na matatizo ya vidonda vya tumbo, maradhi
yaliyopelekea kulazwa katika hospitali ya Mwananyamala Dar es salaam.
Kardinali
ambaye pia ni mjomba wake, amesema kuwa Ndanda alihamishiwa katika
Hosptali ya Taifa Muhimbili siku mbili zilizopita kutoka Mwananyamala
baada ya tatizo lake kushindikana kabla ya mauti kumkuta majira ya saa
mbili asubuhi ya leo.
"Nilikuwa
naye hospitali tangu jana, na nimekesha naye, ilipofika asubuhi hali
yake ilikuwa nafuu, nikaondoka kurudi nyumbani kwa ajili ya chakula,
nikaacha anafanyiwa mpango wa damu maana alikuwa amepungukiwa damu,
lakini muda mfupi baada ya kuondoka hospitali hapo nikapigiwa simu kuwa
Ndanda amefariki, ilikuwa mida ya saa 2 asubuhi” Amesema Gento.
Gento amesema taratibu za mazishi zinasubiri mama yake arudi Dar es salaam, ndipo wataamua kama asafirishwe au azikwe huku
“Mama
yake alikuwa amekwenda Lubumbashi, lakini sasa inabidi ageuze na ndege,
akisharudi ndiyo tutajua kama tunazika au tunasafirisha…… mama yake ni
dada yangu, kwahiyo Ndanda ananiita mimi mjomba”
Hadi
mauti yanamkuta Ndada alikuwa akifanya shughuli za muziki kama msanii
wa kujitegemea ‘Solo Artist’ pamoja na shughuli za kibiashara
0 comments:
Post a Comment