Watahiniwa
74,920 leo wanaanza kufanya mtihani wa kuhitimu Kidato cha Sita katika
shule mbalimbali nchini huku watahiniwa 11,597 wakifanya mtihani wa
Ualimu.
Ofisa
Habari wa Baraza la Mitihani (NECTA), John Nchimbi amesema kuwa mtihani
wa kidato cha sita unaanza leo hadi Mei 19, mwaka huu.
Nchimbi
amesema kati ya watahiniwa hao waliosajiliwa, watahiniwa 65,610 ni
watahiniwa wa Shule huku watahiniwa wa Kujitegemea wakiwa 9,310.
“Kati
ya watahiniwa wa shule 65, 610, watahiniwa wasichana ni 24,549 na
wavulana ni 41,061 huku watahiniwa wa kujitegemea wasichana wakiwa ni
3,176 na wavulana ni 6,134,” alisema Nchimbi.
Kwa
upande wa mtihani wa ualimu, Nchimbi amesema kati ya watahiniwa 11,597
watakaofanya, watahiniwa 10,942 wanafanya Ualimu Daraja A na watahiniwa
654 wanafanya mtihani wa Stashahada ya Sekondari na mmoja anafanya
Stashahada ya Ufundi.
“NECTA
inatoa mwito kwa kamati za mitihani za mikoa, na wilaya kuhakikisha
kuwa taratibu zote za mitihani zinazingatiwa ipasavyo ikiwa ni pamoja na
kuhakikisha mazingira ya vituo vya mitihani yapo salama, tulivu na
kuzuia mianya yote inayoweza kusababisha udanganyifu.
“Kwa
wanafunzi tunaamini walimu wamewaandaa vizuri, na ni matarajio yetu
wanafunzi watafanya mitihani yao kwa kuzingatia taratibu zote za
mitihani ili matokeo ya mitihani yaoneshe uwezo wao halisi kulingana na
maarifa na ujuzi waliopata katika kipindi walipokuwa shule,” aliongeza Nchimbi.
Aidha,
Nchimbi alitoa mwito kwa jamii kutoa ushirikiano unaotakiwa kuhakikisha
mtihani unafanyika kwa amani na utulivu na kusisitiza kuwa mtu
asiyehusika na mtihani asiingie kwenye eneo la mtihani.
0 comments:
Post a Comment