Habari Mpya

Wednesday, June 08, 2016

Historia ya Mwanamuziki Mashuhuri Ntokozo Mbambo

Ntokozo Mbambo alizaliwa mwaka 1985 Kwa Zulu Natal nchini Afrika ya kusini na toka akiwa mdogo alipenda sana Kuimba.Ntokozo aliolewa mwaka 2008 na mwanamuziki maarufu na producer mahili nchini humo Nqubeko Mbatha na wamebahatika kupata watoto wawili wa kike ambao kwa pamoja wanaishi jijini Johanesberg nchini Africa ya Kusini.

Hosanna Kwanza
Ntokozo akiwa on Stage
Kipaji chake cha kuimba kiliibuliwa na wazazi wake (Mr & Mrs J Mbambo)  ambao walimpa nafasi ya kuimba katika timu ya kusifu na kuabudu katika kanisa waliokuwa wakiabudu.

Mwaka 2001 akiwa na miaka 15 tu  alijiunga na Joyous Celebtration na kumfanya kuwa mwanamuziki mdogo kabisa katika kundi hilo.Mwaka huohuo wa 2001 alifanikiwa kutoa album ilifanya vyema sana iliyoitwa “Bembelea” na ilipotimu mwaka 2007 Ntokozo alifanikiwa kutengeneza Live DVD album iliyoitwa Keep on Belieiving.

Album hiyo ilikuwa produced na Nqubeko Mbatha ambaye baadaye alikuwa mumewe baada ya wawili hao kufunga ndoa mwaka 2008.

Wimbo wa Keep on Beleiving ulifanikiwa kupata tuzo ya  Album bora ya mwaka kutoka kituo cha redio cha Metro Fm. Mwaka 2008 wimbo huo  pia ulimuingiza Ntokozo kwenye  mchakato wa kuwania tuzo katika vipengele vitatu tofauti ndani ya tuzo za Crown  Gospel Music Awards .

Ntokozo kupitia ziara maalumu ya kimuziki nchini humo alifanikiwa kuimba jukwaa moja sambamba na wanamuziki nguli wa Gospel duniani akiwemo Yolanda Adams, Donnie McClurkin, Kirk Franklin and Cece Winans on their South African tours respectively.
2Ntokozo na Nqubeko wakiwa na baadhi ya Tuzo zao
Mwanamama huyu pia amefanikiwa kuhudumu katika nchi mbalimbali duniani kuhudumu ikiwemo Ghana,Kenya, USA,Swaziland,Botswana,Uingereza pamoja na nchi nyingine nyingi.

Ntokozo Mbambo mwaka 2012 ikiwa ni miaka 11 tangu yeye na muwewe wajiunge Joyous Celebration waliamua kuondoka kundini humo na kuanza kufanya kazi zao binafsi kama Solo artists,ni Ntokozo ambaye alianza kutoka kisha baada ya wiki mbili mumewe Nqubeko naye alitangaza uamuzi huo kupitia page yake ya facebook.
DSC_0375_1 The Mbathas
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

0 comments:

Item Reviewed: Historia ya Mwanamuziki Mashuhuri Ntokozo Mbambo Description: Rating: 5 Reviewed By: mcjohnminja.blogspot.com
Scroll to Top