Jikumbushe haya kuhusu ndoa:
1. Ndoa ni agano la milele mpaka kifo (ajiandae kwa hilo kiakili, kiufahamu, kihisia na kiroho)!
Ukikurupuka kama fashion au kufikiri ni mahali pa kulala na kula bata, wafaaa!
2. Ni muhimu ujue ndoa ni vita ya kuhakikisha “hamshindwi na kuachana kama wengine” bali mnaishi kuweka mfano na msingi kwa vizazi vingi vijavyo!
Ujue unawajibika kupigana na kuliokoa jahazi la ndoa mpaka pumzi yako ya mwisho.
Ni vita ambayo hauruhusiwi kuinua mikono juu kusurrender.
Mpaka unakata pumzi unawajibika kuhakikisha “agano umelilinda” na umepiga vita vizuri mbele za Mungu na wanadamu.
3. Ujue future nzuri au mbaya za vizazi vingi vijavyo zinategemea uimara na kudumu kwa ndoa yako.
Ujue ndoa si mchezo wala lelemama.
Ukikwama wewe kukaa na ndoa yako, umepitisha mateso kwa vizazi vingi vijavyo.
Si sherehe ya harusi wala pete ama zawadi zinazotolewa siku ya harusi.
Ujue ni jukumu la ajabu linalogharimu uhai wako, mpaka unaondoka duniani.
Mtu akijua hii kitu na akajipanga hakuna talaka wala kuachana.
Ndoa zinavunjika kwa sababu “hazikuandaliwa” yaani wanandoa walifikiri kwamba hakutakuwa na upepo, mvua na dhoruba… Hivyo hawakuandaa silaha wakati wa amani.
Matokeo yake wakikutana na picha tofauti na vigelegele na nderemo, wanaamua kuachia ngazi.
Hakuna kitu kibaya kama kutembea kwenye bustani nzuri mno ambayo ndani yake wamo wadudu wanaouma na wanaoudhi lakini ulichoambiwa mwanzo ni bustani nzuri mno bila kujulishwa kuhusu wadudu wasumbufu waliomo bustanini wa kuwaepuka!
Kama uko kwenye ndoa na tayari umekutana na wadudu na haukubeba dawa ya kuua wadudu, HAKUNA MUDA WA KURUDI MWANZO kuchukua dawa.
Hapohapo ulipo anza kukusanya dawa kupitia MAARIFA YA NENO NA VITABU NA SEMINA ZA WANANDOA WALIOFAULU KWA MIAKA KADHAA ZAIDI YAKO.
Lakini usikubali kuipoteza bustani yako nzuri ya ndoa.
Ulichokiona siku ya harusi ni “uzuri wa bustani” ambao unaweza kurudi kama utajifunza kuua wadudu wakali walio bustanini.
Mungu akusaidie uliyemo ndani ya ndoa akupe hekima na maarifa ya kukuganya ukanyage nyoka na ng’e na nguvu zote za adui humo bustanini.
Tulio nje ya ndoa… Usijidanganye nyakati zimegeuka.
Hautaingia kichwakichwa kama mama yako au baba yako na ukabaki salama.
Maarifa yapo tayari, hakikisha umebobea na kuiva kwa maarifa na siri nyingi kuhusu taasisi hii kubwa na muhimu ya Mungu.
Soma vitabu, hudhuria semina, soma Biblia yako na hakikisha kila mahali penye masuala ya ndoa, mme na mke, mahusiano, kote umepaelewa na kuanza kuyatenda.
“Kwa mashauri mengi wokovu huja”
Pia “Kwa mashauri mengi fanya vita”
Usikurupuke, hakikisha unajua walau MAMBO YA MSINGI kuhusu mme/mke.
Na ujipange kuyakabili na kushinda.
Nje ya hapo u-sister na u-paroko unakufaa zaidi!
Ni kweli pekee ndiyo inatoa uhakika wa uhuru!
Mwl D.C.K www.yesunibwana.org

0 comments:
Post a Comment