Christina Shusho amesema hapa nchini hakuna sababu ya msingi ya
watanzania kutokuwa na Tuzo za Muziki wa Injili. kupitia
kipindi cha Gospel Track cha Clouds Fm kinachoongozwa Harris Kapiga
Shuhso amesema wale wadau ambao wako mstari wa mbele kwenye muziki wa
injili nchini bado wamelala.Shusho amaesema wadau wote wamezamia kuwa ma
Motivational Speakers na Ma Mc badala ya kuiinua industry ya Muziki wa
injili nchini.
Christina amesema badala ya kutafuta suluhisho la muziki wa injili nchini wadau wengi wamebaki kutafuta urahisi tu.Akitolea mfano wa wadau wa injili walioko Clouds Media Group (Samuel Sasali, Hadson Kamoga, Harris Kapiga, na Jimmy Temu) amesema wadau hawa wapo kwenye Media inayofanya vizuri sana nchini lakini ninyi mpo tu mmekaa tu mmekalia kuwa ma Mc na ma motivational Speakers aiseeee Bwana awaone”

Harris Kapiga
Muongozaji wa kipindi hicho Harris Kapiga alikubali 100% alichokisema
Shusho kuwa ni kweli, Kwa mtazamo wake Harris amesema kikubwa
kinachopelekea hali hiyo kwa wadau hao ni kitendo cha kila mmoja wao
kutotaka kuwa chini ya mwenzake,yaani kila mtu anafanya vitu kivyake
vyake na kutotaka kuwa na kitu cha pamoja.Akitolea mfano wa nchi ya
Kenya Shusho amaesema kinachopelekea industry ya Kenya kuwa nzuri ni
watu wakawaida ambao wanaadaa matamasha kila weekend.
Hadson Kamoga
Shusho alialikwa redioni na Harris Kapiga
kuelezea namna alivyopokea ushindi wake wa Tuzo za Groove awards 2016
ambapo ameibuka kuwa mwanamuziki bora wa nyinbo za Injili kwa nchi za
Afrika Mashariki na kati.Sambamba na hilo shuhso ameelezea namna
alivyokatisha Ziara yake nchini Marekani iliyodumu kwa siku tatu tu
nakurudi nchini Kenya alikoalikwa na Raisi wa Nchi hiyo Mh Uhuru Kenyata
katika sherehe maarufu nchini humo za Madaraka’s Day.
0 comments:
Post a Comment