Katibu
Mkuu Wizara ya Ardhi,Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Yamungu
kayandabila amesema kuwa serikali iko mbioni kuunda chombo cha kudhibiti
upandaji wa kodi za nyumba za kupanga.
Dkt
Kayandabila ameyasema hayo jana jijini Dare s Salaam alipokuwa
akizungumza katika kipindi cha asubuhi cha Power Breakfast kinachorushwa
na Clouds Fm.
“Sisi
kama serikali tumesikia kilio cha wapangaji na tuko mbioni kumaliza
tatizo hili kwa kuunda chombo kitakachodhibiti upandaji wa kodi hizi za
nyumba kiholela,tumeshapokea kesi nyingi sana kutoka kwa wananchi na
hivyo tumejipanga kulitatua kabisa tatizo hili”Alisema Dkt Yamungu.
Aidha
katibu mkuu huyo amewaasa wapangaji wa nyumba za kupanga kuhakikisha
wanakuwa na mikataba ya kisheria yenye makubaliano ya pande zote mbili
kupunguza migongano isiyokuwa ya kilazima na kushauri kama watashindwa
kumudu gharama za mwanasheria wanaweza kuwatumia wenyeviti wa serikali
za mitaa kama mashaidi katika kusaini mikataba yao.
Awali
ya yote Dkt Yamungu alizungumzia kukamilika kwa Sera ya nyumba ambayo
iko mbioni kukamilika ikizungumzia masuala haya yote na kwa kiasi
kikubwa sera hii itapunguza migogoro mingi ya masuala ya nyumba kwa
ujumla.
Mwaka
huu mwezi wa nne Waziri wa Ardhi,Nyumba na Maendeleo ya Makazi
Mhe.William Lukuvi aliweka wazi Bungeni nia ya serikali kutungwa kwa
sheria itakayounda chombo cha kudhibiti upandaji wa kodi za nyumba za
kupanga.
0 comments:
Post a Comment