Habari Mpya

Friday, June 03, 2016

Mwenyekiti Wa Kamati Ya Uchaguzi Ya TFF Abwaga Manyanga, Asema Hatosimamia Uchaguzi Wa Yanga

MWENYEKITI wa kamati ya uchaguzi ya TFF Wakili Aloyce Komba ameamua kujitoa katika kuratibu na kusimamia mchakato wa uchaguzi wa klabu ya Yanga uliopangwa kufanyika tarehe 25 June 2016 na zaidi ametoa sababu 6 zilizomfanya aamue kujiweka pembeni kwenye mchakato huo.

Sababu zilizomfanya Wakili huyo kuachia ngazi ni kama ifuatavyo;

1. Katika mchakato huo nimetuhumiwa kupanga kumhujumu kwa kukata jina la mmoja wa wagombea nafasi ya uenyekiti Bw. Yusuf Manji. Tuhuma ambazo zilitolewa tarehe 2 June kwa waandishi wa habari.

2. Kutokana na tuhuma hizo, Yusuf Manji amesema ni moja ya sababu zilizomfanya achukue fomu za kugombea uchaguzi utakaoratibiwa na Yanga.

3.Tuhuma hizo ambazo ni kubwa kwangu binafsi na zikigusa taaluma yangu ya sheria zimetolewa wakati klabu ya Yanga inahitaji amani, utulivu na mshikamano mkubwa wa wanachama, wapenzi na washabiki wake, hivyo mimi kutokuwa chanzo chochote cha vurugu zinazoweza kutokea.

4. Tuhuma hizo zinahusu mimi kupewa fedha za hongo au rushwa (kiasi hakijulikani) ili nishawishi wajumbe wenzangu wa kamati ya uchaguzi ya TFF kukata jina la aliyekuwa mgombea mtarajiwa, Bw. Yusuf Manji kwasababu ambazo hazijaelezwa.

5. Napaswa kupisha uchunguzi wowote huru wa tuhuma hizo nzito kama zimeshafikishwa katika vyombo vya uchunguzi wa masuala ya rushwa ili mimi nipate fursa ya kujitetea kwa uhuru zaidi.

6.Kwa kuzingatia ushauri wa watu mbalimbali ninaowaheshimu na kuwapenda sana ndani na nje ya klabu ya Yanga hususani wanasheria wengine nguli wa masuala ya michezo kama vile Wakili Sais Hamad El-Maamry, Wakili Sam Mapande, Wakili Alex Mgongolwa na waandishi wa habari waandamizi wa michezo, nimeona nisishiriki mchakato huu kwa kusimamiwa na TFF au hata ukisimamiwa na klabu ya Yanga yenyewe.

Kwakuwa mimi ni muumini mkubwa wa utawala wa sheria na hasa masuala ya katiba na demokrasia katika vilabu na vyama vya michezo, napaswa kuanzia sasa kutoshiriki vikao vyote vinavyohusu mchakato wa klabu ya Yanga nikiwa kama Mwenyekiti au Mjumbe.

Nawaomba Rais wa TFF, Bw. Jamal Malinzi na Katibu Mkuu Selestine Mwesigwa na wajumbe wenzangu wa kamati ya uchaguzi ya TFF, nimemuachia madaraka ya kuratibu na kusimamia uchaguzi wa klabu ya Yanga, Wakili Domina Mideli, ambaye ni Makamu Mwenyekiti wa kamati hiyo.

  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

0 comments:

Item Reviewed: Mwenyekiti Wa Kamati Ya Uchaguzi Ya TFF Abwaga Manyanga, Asema Hatosimamia Uchaguzi Wa Yanga Description: Rating: 5 Reviewed By: mcjohnminja.blogspot.com
Scroll to Top