Mke
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mama Janeth Magufuli
ameahidi kundelea kusaidia kambi za wazee na watu wenye ulemavu ikiwamo
ukoma kutokana na kundi hilo kusahaulika kwa muda mrefu.
Mama
Janeth ameyasema hayo wakati wa hafla ya utoaji wa Msaada wa vyakula,
Mafuta kwa ajili ya watu wenye ulemavu wa ngozi pamoja na madawa katika
kambi ya wazee na watu wenye ulemavu ya Nandanga iliyopo Wilayani
Ruangwa Mkoani Lindi.
Aidha
Mama Janeth Magufuli amesema kuwa kwa kutambua umuhimu wa kundi hilo
mpaka sasa kwa kushirikiana na wadau wengine ameshatoa Misaada katika
Kambi 4 za Mikoa ya Dar es Salaam (NUNGE) Mwanza (BUKUMBI), Lindi
(NANDANGA) na Mtwara (NKASEKA) ambayo inathamani ya takribani shilini
Milioni 250.
Katika
hatua nyingine Mama Janeth Magufuli alizindua jiwe la msingi kwenye
Jengo la Zahanati Zahanati ya Nandanga itakayorahisisha upatikanaji wa
huduma ya afya kwa wakazi wa eneo hilo waliokuwa wakisafiri umbali mrefu
kufuata huduma hiyo.
Naye
Mke wa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mama Mary
Majaliwa amemshukuru Mama Janeth kwa uamuzi wa kutembelea kambi hiyo na
kuwaomba wadau wengine kujitokeza kumuunga mkono ili kusaidia watu wenye
ulemavu na wazee.
Akiongea
kwa Niaba ya Wazee wa Kambi ya Nandanga Mratibu wa Kambi hiyo Bw.
Agnerus Chiamba alimshukuru Mama Janeth Magufuli kwa Misaada hiyo kwani
itawasadia kwa kiasi kikubwa kutokana na uhitaji waliokuwa nao.
0 comments:
Post a Comment