Habari Mpya

Tuesday, June 07, 2016

Rais Magufuli ahudhuria Ibada kwenye kanisa la Mzee wa Upako

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania leo amelitembelea kanisa la maombezi linaloongozwa na Anthon Lusekelo maarufu kama Mzee wa Upako eneo la Ubungo Jijini Dar es salaam

Akizungumza katika kanisa hilo Rais Magufuli amesema kwamba serikali yake itajenga barabara kutoka Ubungo Kibangu hadi River Side ambayo itaungana na barabara ya Mandela.

Rais Magufuli amewaambia waumini wa kanisa hilo kwamba amepita katika barabara hiyo ili kujionea hali halisi ambayo waumini hao huwa wanapita wakielekea katika ibada.

Aidha Rais Magufuli amempongeza Kiongozi wa Kanisa hilo Anthon Lusekelo kwa namna anavyotoa mahubiri yake kwa waumini na watazamaji ambao hufuatilia runinga.
2(7)
Rais Magufuli akaiwa na Mzee wa Upako na Mkewe mama Janet Magufuli kanisani Ubunbo kibangu kwa Mzee wa Upako

‘’Mimi ni mfuatiliaji mzuri sana wa mahubiri yako, kwa hiyo mahubiri unayotoa yanasambaa, kwa kweli mimi na familia yangu huwa tunabarikiwa sana, kwa hiyo nataka kukuhakikishia ninakupenda sana’’-Amesema Rais Magufuli.

‘’Ndiyo maana kuna siku ulizungumzia barabara yako ikabini nitafute mbinu za kuweza kuishughulikia kwa njia ya wazi nikamuagiza meneja wa barabara Mkoa wa Dar es salaam akajakuitizama nakufahamu changamoto zilizopo na kufanya upembuzi yakinifu nataka kukuhakikishia fedha za ujenzi wa barabara hii zipo’’-Amesema Rais Magufuli.

Kwa upande wake kiongozi wa kanisa hilo Anthon Lusekelo amemshukuru Rais Magufuli kwa kutembelea kanisa hilo na kumtakia kheri katika uongozi wenye maendeleo hususani kujenga viwanda.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

0 comments:

Item Reviewed: Rais Magufuli ahudhuria Ibada kwenye kanisa la Mzee wa Upako Description: Rating: 5 Reviewed By: mcjohnminja.blogspot.com
Scroll to Top