Habari Mpya

Friday, June 17, 2016

Ucheagu asema anatamani kufanya Kolabo na Cece Winans

Mwanamuziki Uche agu maarufu kama Uche Double Double amesema kwa sasa anatamani kufanya Colabo na Mwanamuziki Cece Winans kutoka nchini Marekani.

Uche alizungumza hayo wakati akihojiwa na mtangazaji wa DutchesTv. Uche  mkwa sasa anatarajia kuachia album yake mpya aliyoipa jina la The Glory Experience mnamo tarehe 24/6/2016. 

kuhusu Cece winans Uche alifunguka kuhusu hilo mara baada ya kuulizwa kwa sasa duniani ni mwanamuziki gani amabaye unapenda kufanya naye kazi.
NASHVILLE, TN - JANUARY 18: CeCe Winans performs at the 14th annual BMI Trailblazers of Gospel Music Awards at Rocketown on January 18, 2013 in Nashville, Tennessee. (Photo by Erika Goldring/Getty Images)
Cece Winans
Baada ya swali hilo Uche alienda Straight na kumtaja Cece Winans, sababu za kumtaja Cece Winnas Uche amesema Cece amekuwa pale(Top)  siku zote licha ya umaarufu wake wote na ni kwa sababu ya tabia yake(Character).Katika mazungumzo hayo uche amaesema amewahi kukutana na Cece na kuongea. 

Uche akasema hata Cece Winans aliwahi ulizwa na kituo kimoja cha redio ni nani kutoka Afrika anatamani kufanya nae kazi akanitaja mimi, hili sikulijua na hata yeye hakuwahi kujua kuwa natamani kufanya naye Colabo.

Kuhusu album yake mpya Uche amesema ametumia maproducer  na watu wenye vipaji vya hali ya juu ambao wamewahi kufanya kazi na Israel Huston, na William McDowell.Let us wait for his new coming.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

0 comments:

Item Reviewed: Ucheagu asema anatamani kufanya Kolabo na Cece Winans Description: Rating: 5 Reviewed By: mcjohnminja.blogspot.com
Scroll to Top